Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKAZI WA MBEYA WAIOMBA TCRA KUTOA ELIMU YA UTUMAJI USAFIRISHAJI WA MIZIGO NA VIPETO

Na Mwandishi Wetu, Mbeya

WAKAZI wa mkoa wa Mbeya wameiomba Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) kusambaza zaidi elimu juu ya utumaji rasmi wa mizigo na vifurushi ili kuwanusuru wananchi wengi zaidi na upotevu wa mizigo.


Wakizungumza katika kampeni ya wazi ya uhamasishaji wa matumizi ya watoa huduma rasmi wakati wa kutuma mizigo wananchi hao wamesema mizigo migo inapotea kutokana na kutojua taratibu rasmi za kuwatambua watoa huduma wenye leseni.


Akizungumzia elimu hiyo mfanyabiashara Anangisye Mwakyoma amesema mara nyingi anapotaka kutuma mizigo huangalia basi ambalo analijua lakini baada ya kupata elimu hii atazingatia maelekezo ambayo yametolewa.


Akizungumzia faida ya elimu Bibi kisa Mwaipyana amesema iwapo angepata elimu hii tokea awali asingepoteza mzigo ambao alituma kwenye basi kupitia wakala ambaye hakuwa na ofisi.


Mch Elibariki Mmari ameishauri TCRA kuweka wazi sifa na vigezo vya wasafirishaji rasmi ili wananchi wawe wanaangali hivyo kabla ya kutuma mizigo yao.


Awali akitoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kutumia watoa huduma wenye leseni wakati wa kusafirisha mizigo Meneja wa TCRA wa kanda ya nyanda za juu kusini Mha. Asajile John amesema TCRA inapotoa leseni hutoa pia masharti na vigezo ambavyo watoa huduma hao hutakiwa kuvizingatia.


Amevitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na kampuni kiwa ofisi rasmi na kutoa risiti wanapoagiza ya mizigo wanauosafirisha.


Elimu hii ni sehemu ya kampeni ya tuma chap kwa usalama inayoendeshwa na TCRA nchi nzima kuelimisha wananchi umuhimu wa kutumia wasafirishaji wa mizigo waliosajiliwa.
Meneja wa Nyanda za Juu Kusini wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) Mhandisi Asajile John akizungumza na wananchi wa Jiji la Mbeya kuhusiana Utumaji wa Vifurushi na Vipeto ikiwa ni Kampeni ya TCRA Tuma Chap kwenye viunga vya jiji hilo la Mbeya.
Afisa Habari na Uhusiano Mwandamizi Mkuu Mabel Masasi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA) akigawa vipeperushi kwenye basi la Abiria (Daladala) Jijini la Mbeya ikiwa ni kampeni ya Tuma Chap ya Utumaji wa Vifurushi na Vipeto kwenye viunga vya jiji hilo la Mbeya.
Wananchi wakiangalia simu baada ya kupewa elimu kuhusianq na utumaji wa vifurushi na vipeti jijini Mbeya.
Afisa mkuu wa Abel John Masuala ya posta wa TCRA akitoa elimu kuhusiana na usafirishaji wa vifurushi na na Vipeto katika Viunga vya Mbeya ikiwa ni Kampeni ya TCRA Tuma Chap


Post a Comment

0 Comments