Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO ATOA POLE MSIBA WA MTOTO WA MALECELA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimfariji na kutoa rambirambi kwa Waziri Mkuu Mstaafu John Malecela, kufuatia kifo cha mtoto wake marehemu William Malecela aliyefariki dunia Mei 14, 2023. Waziri Jafo alifika nyumbani kwa Mzee Malecela Uzunguni Jijini Dodoma leo Mei 16, 2023 kumwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Isdor Mpango. Katikati ni Mhe. Anne Kilango Malecela, Mke wa Mzee Malecela.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akimwakilisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango kusaini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha aliyekuwa mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela, marehemu William Malecela aliyefariki dunia Mei 14, 2023, wakati Waziri Jafo alipofika nyumbani kwa Mzee Malecela Uzunguni jijini Dodoma leo Mei 16, 2023.

(PICHA NA OFISI YA MAKAMU WA RAIS)

Post a Comment

0 Comments