NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga Sc imefanikiwa kutinga fainali Kombe la Shirikisho la Azam mara baada ya kuichapa Singida Big Stars 1-0 kwenye mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Liti mkoani Singida.
Yanga Sc iliweza kuwapa nafasi wachezaji wengi ambao mara nyingi wamekuwa hawaanzi kwenye mechi akiwemo Mauya, Doumbia, Mzize na mlinda lango Metacha Mnata.
Katika mchezo huo ambayo ilikuwa ya aina yake, timu zote zilitengeneza nafasi za magoli kipindi cha kwanza bila mafanikio, hivyo kwenda mapumziko matokeo yakiwa 0-0.
Yanga ilifanya mabadiliko kadhaa kwa baadhi ya wachezaji, wakaingia Fiston Mayele, Tuisila Kisinda, Dikson Job pamoja na Musonda mabadiliko hayo yalizaa natunda kwani Yanga ilianza kulisakama lango la wapinzani na kufanikiwa kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao hatari Fiston Kalala Mayele na matokeo kuwa 1-0.
Yanga Sc inaenda fainali ambapo inaenda kukutana na Azam Fc ambao walitinga hatua hiyo mara baada ya kuwaondoa Simba Sc.
Mechi hiyo ya Fainali itechezwa katika dimba la Mkwakwani Tanga hivi karibuni.
0 Comments