Ticker

6/recent/ticker-posts

DENI LA SERIKALI LAONGEZEKA KWA ASILIMIA 13.9% IKILINGANISHWA NA MWAKA 2022

NA EMMANUEL MBATILO

Hadi kufikia mwezi Aprili 2023, deni la Serikali lilikuwa shilingi bilioni 79,100.19 sawa na ongezeko la asilimia 13.9 ikilinganishwa na Shilingi bilioni 69,440.01 kwa kipindi kama hicho mwaka 2022.

Akizungumza wakati akiwasilisha taaifa ya hali ya Uchumi katika Mwaka 2022 leo Juni 15,2023 Bungeni Dodoma,Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba amesema ya kiasi hicho, deni la nje ni shilingi bilioni 51,162.60 na deni la ndani ni Shilingi bilioni 27,937.59.

"Ongezeko la deni limetokana na: kupokewa kwa fedha za mikopo kwa ajili ya kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya barabara, reli, viwanja vya ndege, umeme, elimu na afya". Amesema Dkt. Nchemba

Aidha, amesema kuwa Tathmini ya uhimilivu wa deni la Serikali iliyofanyika Desemba, 2022 imeonesha kuwa deni ni himilivu na viashiria vya deni viko ndani ya wigo unaokubalika kimataifa katika kipindi cha muda mfupi, wa kati na mrefu.
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akiwasilisha Bajeti Kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, Bungeni jijini Dodoma, Juni 15, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, akionesha Bajeti kuu ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024, wakati akiwasilisha Bajeti hiyo, Bungeni jijini Dodoma, Juni 15, 2023. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Post a Comment

0 Comments