Ticker

6/recent/ticker-posts

MENEJA BANDARI ZA ZIWA TANGANYIKA AANIKA MAAFANIKIO LUKUKI BAADA YA MABORESHO YA MIUNDOMBINU YA BANDARI

Na Mwandishi wetu, Kigoma

MAMLAKA ya Bandari ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeeleza kwamba imewekeza zaidi ya Sh.bilioni 800 kwa ajili kutekeleza miradi ya kuboresha bandari nchini kwa lengo la kuongeza utendaji kazi ukiwemo wa kuhudumia mizigo na abiria.

Pia imesema kwa upande wa Ziwa Tanganyika, mamlaka hiyo imewekeza Sh. bilioni 100 ili kuboresha bandari za ukanda wa ziwa hilo ambazo zimekuwa zikituma kutoa huduma ya kusafirishia abiria na shehena ya mizigo kwenda nchi jirani

Akizungumza leo Juni 2, 2023, Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula pia amesema bandari ya Kigoma ndio bandari kongwe na kubwa kuliko bandari zote za ukanda wa Ziwa Tanganyika na hadi kufikia Mei,2023 imehudumia tani 131,000 ya shehena ya mzigo.

Amefafanua idadi hiyo ni sawa na asilimia 48 ya shehena zote zinayohudumiwa katika bandari zote za ukanda wa ziwa hilo zipatazo tani 273,000 na kusisitiza bandari ya Kigoma imewezesha kupunguza msongamano wa mizigo bandari ya Dar es Salaam.

Mabula amesema asilimia 80 ya mizigo inayohudumiwa bandari ya Dar es Salaam inakwenda nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na katika mizigo hiyo, asilimia 48 husafirishwa kupitia bandari ya Kigoma.

Pamoja na hayo ametoa rai kwa wadau wa bandari na sekta binafsi kuchangamkia fursa zinazotokana na uboreshaji wa bandari za Ziwa Tanganyika ambao unafanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari.

Kwa upande wake Mhandisi wa mradi wa uboreshaji wa bandari za Kibirizi na Ujiji, Mhandisi Elly Mtaki amewaambia waandishi wa habari kwamba baada ya kukamilika kwa mradi huo ufanisi utaongezeka katika upakuaji na upakiaji wa mizigo. "Na hiyo ni kutokana na ujenzi wa gati jipya linalojengwa katika bandari ya Kibirizi."

Wakati huo huo baadhi ya mawakala wa forodha kwenye bandari hiyo wamefurahia utolewaji wa huduma ambao wamesema uboresha na hiyo inatokanana uwekezaji ambao umefanywa na Serikali kupitia TPA.
Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Edward Mabula akiwaelezea utendaji kazi wa bandari za ukanda wa ziwa Victoria
Mbaraka Said ambaye ni Wakala wa Forodha katika bandari ya Kigoma akiongea na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wao katika bandari ya Kigoma
Wakala wa Forodha katika bandari ya Kigoma, Brian William akiongea na waandishi wa habari kuhusu utendaji kazi wao katika bandari hiyo leo Juni 02, 2023
Mhandisi wa Mradi wa uboreshaji wa bandari za Kibirizi na Ujiji, Mhandisi Elly Mtaki akiwaelezea waandishi habari maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo leo Juni 02, 2023
Mwonekano wa ujenzi wa gati jipya katika bandari ya Kibirizi iliyopo katika manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma ukiwa unaendelea
Post a Comment

0 Comments