Ticker

6/recent/ticker-posts

WAJASIRIAMALI WA BIDHAA ZA MAZIWA WAASWA KUZALISHA BIDHAA ZENYE UBORA


Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Bw. Daniel Marwa akiwatembelea wazalishaji, wasindikaji, na wasambazaji wa bidhaa za maziwa na wajasiriamali kwa ujumla waliofika katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa, mkoani Tabora .

************

Wajasiriamali wa bidhaa za maziwa nchini wameaswa kuzalisha bidhaa zenye ubora ili kuweza kuhimili ushindani katika soko la ndani na kimataifa.

Haya yamesemwa na Bw Daniel Marwa, Afisa Udhibiti Ubora (TBS) wakati akiwatembelea washishiriki wa maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Maziwa kitaifa yaliyofanyika Tabora katika mabanda yao.

Bw. Marwa alitumia fursa hii kutoa elimu kuhusu masuala ya viwango, namna bora ya uzalishaji wa bidhaa kwa ukizingatia namna bora ya usafi lengo likiwa ni kuzalisha bidhaa bora na salama kwa watumiaji wa mwisho.

Pia alipata nafasi za kuwaeleza namna wanavyoweza kupata alama ya ubora kwa kutumia huduma ya uthibishaji ubora wa bidhaa bila gharama yoyote kwa wajasiriamali kwani serikali kila mwaka hutengenga fedha ili wajasiriamali wadogo na wa kati wathibitishe ubora wa bidhaa zao ili waweze kufikia makoso makubwa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Afisa Masoko (TBS), Bi. Rhoda Mayugu amesema, TBS ilitumia maonesho hayo kuwaelimisha wananchi kuhusu faida na umuhimu wa kununua bidhaa zilizothibitishwa ubora wake pamoja na umuhimu wa kuangalia muda wa watumizi wa bidhaa husika kabla ya kununua bidhaa hizo kwani kwa kufanya hivyo hulinda usalama wa afya zao, na kuepuka hasara za kiuchumi zinazoweza kujitokeza

Vita ya bidhaa hafifu sokoni si ya TBS pekee endapo wananchi watashirikiana na TBS kwa kutokununua bidhaa hafifu na kutoa taarifa wanapokutana na bidhaa hafifu ama zile zilizozuiliwa kutumika ni hakika Tanzania haitokuwa na bidhaa hafifu kwani wazalishaji, waingizaji wa bidhaa hizo hawatapata masoko kabisa hivyo kupelekea kuzalisha, kusambaza, kuningiza na kuuza bidhaa bora.



Afisa Udhibiti Ubora (TBS) Bw. Daniel Marwa akiwatembelea wazalishaji, wasindikaji, na wasambazaji wa bidhaa za maziwa na wajasiriamali kwa ujumla waliofika katika maonesho ya maadhimisho ya wiki ya maziwa kitaifa, mkoani Tabora .
TBS imewatembelea wajasiriamali hao kwa lengo la kutoa elimu kuhusu masuala ya viwango na kuwakumbusha kuhusu huduma ya kupata alama ya ubora bila gharama yoyote.

Post a Comment

0 Comments