Ticker

6/recent/ticker-posts

RC FATMA ,WASHIRIKISHE WANANCHI MJUE VIPAUMBELE VYAO KATIKA MIRADI.


Na Shemsa Mussa, Kagera.

Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Fatma Mwassa amesisitiza matokeo bora katika utekelezaji wa miradi ya barabara iliyopo chini ya wakala wa barabara mjini na vijijini TARURA na ushirikishwaji wa wananchi ili kujua vipaumbele vyao kabla ya utekelezaji wa miradi .

Bi Fatma amesema hayo katika kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi yake na kueleza kuwa watendaji wa serikali wapo kwa ajili ya kuwasimamia wananchi hivyo ni vema kutekeleza na kutatua changamoto zao ili kuwaondolea kero mbalimbali pia na kuzingatia ubora na viwango stahiki vya utekelezaji wa miradi.


"Washirikisheni wananchi katika miradi mnayofanya kwao ili nao watoe vipaumbele vyao huwezi kufanya kitu kwa mtu bila kujua yeye anataka nini, na simamieni miradi kwa kujitoa na kwa umakini zaidi, amesema Bi Fatma"


Kwa upande wake katibu Tawala Mkoa Kagera Ndg Toba Nguvila amewasihi watumishi wakiwemo wataalam kutoka TARURA na TANROAD kutoa elimu kwa wananchi kabla ya kuanza utekelezaji wa miradi hiyo ili kuondoa malalamishi ya madai ya fidia pale mirafi inapoanza kutakelezwa.


Nae. Mhandisi wa Wakala wa Barabara za Vijijini na MijinTARURA Mkoa Kagera Bw Avitusi Theodori amesema kuwa Wilaya 5 za mkoa kagera zinatarajiwa kunufaika na mradi wa kuondoa vikwazo barabarani utakaogharimu zaidi ya Bilion 2.5


Adha ameongeza kuwa Halmashauri ya Bukoba mradi huo utahusisha barabara ya katoma -kashozi yenye km 8, Biharamulo barabara ya Runazi -Chebitoke yenye km 4, Karagwe ni barabara inayounganisha kata za Kayanga -Rugela yenye km5, Ngara ni barabara ya Kumwendo -Kigarama -Mkigyango yenye km 11.9, Kyerwa ni barabara ya Kason - Makunyu yenye km 8.

Post a Comment

0 Comments