Ticker

6/recent/ticker-posts

UCHUNGUZI WA KIIKOLOJIA KUHUSU VIRUSI VYA MARBURG WAANZA KAGERA.

Mkurugenzi msaidizi kituo cha maafa ofisi ya waziri mkuu bw prudence wakati wa ufunguzi wa ziara ya uchunguzi
***************************

Na Shemsa Mussa,Kagera.


Wataalam kutoka Wizara za kisekta chini ya Uratibu wa Ofisi ya Waziri Mkuu wameanza uchunguzi wa Kiikolojia kuhusu Ugonjwa wa Virusi vya Marburg baada ya ugonjwa huo kutokomezwa Nchini.


Timu hiyo ya wataalamu inaundwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Ofisi ya Waziri Mkuu ( Menejimenti ya Maafa), Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Afya, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori (TAWIRI), na Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI)


Watalam hao ambao wamekutana Mkoani Kagera wanalenga mufanya uchunguzi wa kiikolojia ikiwa ni utekelezaji wa matakwa ya kimataifa ya kufanyika shughuli mbalimbali za ufuatiliaji baada ya ugonjwa huo kutoweka.


Akizungumza wakati wa ufunguzi wa ziara ya uchunguzi wa kiikolojia Mkurugenzi Msaidizi Kituo cha Operesheni na Mawasiliano ya Dharura Ofisi ya Waziri Mkuu Bw.Prudence Constantine amesema Ofisi ya Waziri Mkuu imeratibu sekta na Taasisi mbalimbali kufanya uchunguzi wa kiikolojia ili kubaini uwepo wa Wanyama wanaoweza kuhifadhi Virusi vya Marburg na mwingiliano wao na binadamu ambapo Uchunguzi huo ni moja kati ya juhudi za pamoja za kuendelea kujua chanzo cha tatizo, kujiandaa, kukabiliana na dharura za kiafya endapo zitajitokeza.

"Wizara ya Afya imeainisha uchunguzi huu kati ya kazi muhimu zinazotakiwa kufanyika ndani ya mpango wa siku 90 wa kurejesha hali Mara baada ya mlipuko wa Marburg ulipotangazwa kuisha hapa kagera".ameeleza Mkurugenzi Prudence .

Akiongea kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Kagera ,Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Issessanda Kaniki amesema baada ya ufuatiliaji wa mbinu za utafiti na vipimo ndani ya siku 42 wameweza kuudhibiti ugonjwa huo hivyo hadi sasa hakuna Mgonjwa hata mmoja.


"Baada ya Ufuatiliaji lakini pia na mbinu mbalimbali za Utafiti Mkoa wa Kagera pamoja na Nchi tunazopakana nazo kwa sasa mlipuko wa Ugonjwa wa Marburg haupo tena".Amesema Dkt, Kaniki.

Uchunguzi huu wa Kiikolojia utakaofanyika kati ya tarehe 12 na 24 Juni, 2023 utahusisha uchukuaji wa sampuli za Wanyamapori, wanyama wa kufugwa pamoja na kufanya utafiti shirikishi jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Muleba na Kyerwa.

Post a Comment

0 Comments