Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAFUNZI WANAOFANYA TAFITI KWENYE JAMII WATAKIWA KUTUMIA TEKNOLOJIA ZINAZOENDANA NA MAPINDUZI YA VIWANDA

WANAFUNZI wanaofanya gunduzi na tafiti zenye lengo la kutatua changamoto mbalimbali katika jamii wametakiwa kujikita zaidi katika kutumia teknolojia zinazoendana na mapinduzi ya nne ya viwanda ikiwa ni pamoja na matumizi ya akili bandia hali itakayosaidia kuongeza umahiri na kuweza kulinda nafasi zao za ajira.

Hayo yamesemwa na Mwanzilishi Mwenza wa Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi (yst) Bw.Gozibert Kamugisha wakati akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa kumekuwa na muamko mkubwa wa wanafunzi kujihusisha na tafiti za kisayansi na ugunduzi nchini ambapo kwa mwaka 2023 wanafunzi takribani 979 wamewasilisha maombi ambapo kati yao tafiti 361 zimepatiwa usaidizi

Aidha amebainisha kuwa baadhi ya kazi za kisayasi zitakazoonyeshwa kwenye maonyesho ya mwaka huu zimejikita katika masuala ya utunzaji wa mazao ya kilimo, utunzaji wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali maji, uzalishaji wa umeme hivyo kuwataka wadau na jamii kwa ujumla kuwaunga mkono wanafunzi hao.

kwa upande wake afisa mtendaji wa Taasisi ya Karimjee Jivanjee Bi.Caren Rowland amesema kuwa taasisi hiyo imeendelea kuboresha program mbalimbali zinazolenga kuwawezesha vijana kufikia ndoto zao ili kuendana na sera ya nchi katika kuleta maendeleo endelevu kupitia uboreshwaji wa miundombinu mbalimbali ya elimu na uwezeshaji na hatimaye kutengeneza kizazi cha wasomi na wabobezi.

Maonyesho ya sayansi na teknolojia kwa mwaka huu yanatarajiwa kufanyika disemba 7 katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam


Post a Comment

0 Comments