Ticker

6/recent/ticker-posts

WASAFIRI WA MAJINI WAPEWA ANGALIZO KUTUMIA VYOMBO VISIVYOSAJILIWA KISHERIA

Afisa Masoko Mwandamizi TASAC, Martha Kelvin akikabidhi zawadi kwa Kaimu Conrad Milinga.
Afisa Mfawidhi TASAC Mkoa wa Tanga, Kapteni Christopher Shalua akitoa maelezo kuhusu TASAC mbele ya Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Conrad Milinga alipotembelea banda hilo.


******************

Na Hamida Kamchalla, TANGA.

WAKALA wa Meli Tanzania (TASAC) imetoa angalizo kwa abiria dhidi ya kupanda vyomo vya usafiri katika maji ambavyo havina leseni na kuambiwa kuwa pamoja na mambo mengine ni kukiuka sheria za usalama baharini.

Kwa mujibu wa Ofisa Mfawidhi wa TASAC Mkoa wa Tanga, Kapteni Christopher Shalua, wasafiri hao sio tu kwamba wanaweka maisha yao hatarini bali pia wanayaweka mashirika ya uokoaji katika hali ya shinikizo.

Kapteni Shalua ameyasema hayo jana wakati akitoa maelezo kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Conrad Milinga aliyetembelea banda la TASAC katika Maonesho ya 10 ya Biashara na Utalii katika viwanja vya Mwahako jijini Tanga kabla ya kuzindua rasmi jana.

Amesisitiza kuwa abiria lazima wazingatie kabisa itifaki zote za kiusalama kwa kupanda meli zilizo na leseni, “siyo kwa usalama wao tu, bali hata kwa usalama wa kila mtu aliye ndani ya vvyombo hivyo,”
alisema.

Aidha Kapteni Shalua amesisitiza umuhimu wa kuhakikisha vyombo vinavyopandishwa vinakuwa na leseni stahiki ili kutoa uzoefu salama kwa abiria wote.

Kwa mujbu wa Kapten Shalua, TASAC imekuwa ikihamasisha kikamilifu
katika Mikoa mbalimbali ya pwani juu ya jambo hilo na kueleza kuwa sababu yake ni rahisi, kwani kabla ya kutekeleza sheria, ni muhimu kuwaelimisha watu.

Amewataka wamiliki na waendesha vyombo vya usafiri wa maji kuzingatia
masharti ya leseni zao kwa kuwanyima abiria nafasi ya kupanda katika
vyombo vya usafirishaji wa mizigo.

Akielezea umuhimu wa Maonesho ya Biashara na Utalii, amesisitiza kuwa
yanatoa fursa ya kipekee ya kuunganishwa na wadau husika na kujenga
uelewa katika masuala mbalimbali yanayohusu usafiri wa maji na
majukumu mengine muhimu yanayotekelezwa na TASAC.

"Ripoti zinaonesha kuwa vyombo vya usafiri wa maji vilivyosajiliwa kubeba mizigo vimeendelea kubeba abiria hivyo kuhatarisha maisha ya watu".

Chini ya kanuni za TASAC, abiria wanapaswa kukataa kupanda vyombo
visivyosajiliwa kupakia abiria na vilivyojaa au kukataa kuoakia kaika
vyomo vinavyoanza safari usiku au vinavyoanza safari katika bandari

Post a Comment

0 Comments