***************
Na Shemsa Mussa, Kagera.
Mkuu wa Mkoa Kagera Mhe Hajjat Fatma Mwassa ameshiriki leo katika dua na kuzungumza na wana kagera katika hafla ya kuupokea mwaka mpya wa kiislamu wa 1445 Hijiria iliyofanyika katika uwanja wa kaitaba ndani ya Manispaa ya Bukoba.
Hafla hiyo ilioandaliwa na Baraza la waisilamu tanzania( Bakwata ) kwa kushirikiana na jumuhiya ya akina mama wa kiislamu tanzania (Juwakita) kwa lengo la kuukaribisha mwaka mpya, kuwapokea na kuwapongeza Mahujaji waliotoka Kuhiji pamoja na kuliombea taifa la tanzania linaloongozwa na Mhe Samia Suluhu Hassan.
Hajjat Mwassa ameanza kwa kuzitaja fadhira( faida)za kwenda kuhiji ikiwemo kuuona Mji wa Makha na Madina, kuizunguka harkahaba na kuingia katika msikiti Mkuu pamoja na kupata swawabu nyingine.
Hajjat Mwassa amechukua nafasi hiyo kuzungumza na wananchi wa mkoa kagera na kusema kuwa bado ana imani na Mkoa wa kagera na ameahidi kutoa ushirikiano katika dini na madhehebu yote kuwaongoza vema bila upendeleo na ubaguzi ili kudumisha amani na ushikamano.
Aidha amesema kuwa zipo changamoto zinazoukabiri mkoa wa kagera ikiwemo suala la Stend ya Mabasi na Maroli pamoja na Soko kuu la Mkoa , amesema matatizo hayo anayafahamu na yamekuwepo kwa muda mrefu hivyo hivi karibuni kila jambo litaanza kutekeleza.
"Naomba wana kagera wenzangu tuweni na subira suala la Stend ya Mabasi kwa mwezi ujao atakuja mtaalam kupima lamani na akimaliza hatuchelewi kuanza ujenzi,amesema Hajjat Fatma".
Hata hivyo Shekhe Mkuu wa Mkoa Kagera Ndg Haruna Kuchwabuta amezishauri na kuzitaka taasisi nyingine pindi likitokea jamboa lolote waweze kutoa taarifa mapema ili nao kama waumin wa dini ya kiisilamu waweze kushiriki na kudumisha umoja na ushirikiano
" jamani nawaambia hapa hatuwezi kufanya lolote likadumu bila amani na kushirikiano wetu ndio nguzo na msingi wa kuwa na amani tujulisheni tutakuja na tutashiriki , amesema Shekhe Kichwabuta".
Nae Katibu wa jumuhiya ya akina mama wa kiislamu tanzania (juwakita ) kwa Mkoa kagera Bi Hashura Hassan Saad Amesema wao kama akina mama wamekuwa wakijitoa na kushiriki katika kazi za jamii ikiwemo kutoa elimu juu ya afya ya lishe , kupinga ukatili wa kijinsia pamoja na kuwaelimisha wanawake juu ya kujishughulisha katika ujasiliamali.
0 Comments