Ticker

6/recent/ticker-posts

JK AKUTANA NA MWENYEKITI WA SENETI WA LESOTHO

Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akies ns Mwenyekiti wa Seneti wa Lesotho Mhe Mamonaheng Mokitimi mjini Maseru siku ya Ijumaa.

Mhe Kikwete yuko katika Ufalme wa Lesotho kwa nafasi yake kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Jopo hili la Wazee wa SADC ambalo Makamu Mwenyekiti wake ni Mheshimiwa Paramasivum Pillay B. Vyapoory, Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Mauritius, limekutana na Serikali na wadau mbalimbali ndani ya Ufalme wa Lesotho, kama mwendelezo wa juhudi ya kusaidia upatitanaji wa utulivu wa kisiasa katika Ufalme huo.

Jopo limekutana na Mhe. Ntsokoane Samuel Matekane, Waziri Mkuu wa Ufalme wa Lesotho; Mhe. Nthomeng Justina Majara, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Sheria na Masuala ya Bunge; Mhe. Tlohang Sekhamane, Spika wa Bunge la Lesotho; Mhe. Mamonaheng Mokitimi, Mwenyekiti wa Seneti; Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Viongozi wa Vyama vya Upinzani; Uongozi wa Ofisi ya Mpito ya Mabadiliko ya Kitaifa (NRTO); Viongozi wa Umoja wa Machifu; na wadau mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments