Ticker

6/recent/ticker-posts

JAMII YASHAURIWA KUTUMIA MCHANGA NA KOKOTO WENYE VIWANGO KWENYE UJENZI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAHITIMU Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, Shule Kuu ya Madini na Miamba(Geo science) Wameanzisha mradi ambao wamefanya tafiti ya madini na miamba ujenzi,baada ya kugundua watanzania wengi wanafanya shughuli za ujenzi bila kujua ubora na viwango vya madini na miamba ujenzi.

Akizungumza katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar es Salaam Muhitimu wa Chuo hicho Bi.Marry Mahenge amesema waligundua kuwa Dar es Salaam na Pwani madini na miamba ujenzi yana udongo mwingi,chumvi na uchafu mwingi hivyo wakapata suluhisho la kuweka mchanga katika viwango vinavyofaa ili kuondoa mipasuko na nyufa katika ujenzi.

Aidha amesema kuwa pia kwa upande wa kokoto,nyingi hazina shida Sana ingawa nyeusi zinaonekana ni imara kwa ujenzi mbalimbali.

"Tunatoa ushauri juu hizo hizo kokoto kwa sababu madini ambayo yamo kwenye hizo kokoto yanaweza kuleta athari fulani au hayafai katika ujenzi wa jengo hilo", Amesema

Amesema wamegundua kwamba watu wengi wanaagiza tu mchanga ambapo unakuta mchanga una madini ndani ambayo yakichanganywa na sementi yanaleta mipasuko na nyufa baada ya ujenzi kwenye nyumba nyingi.

"Nashauri mtu anayetaka kufanya ujenzi apate ushauri kabla ya kufanya ujenzi ni kokoto zipi anatakiwa kuzitumia au mchanga upi utumike katika ujenzi kulingana na bajeti yako ya ujenzi kwa kuzingatia vipimo na kukupa bidhaa ya kusafisha madini ujenzi"alisema

Pamoja na hayo amesema"Sisi tunatoa huduma ya vipimo na ushauri na bidhaa za kwenda kufanyia ujenzi,tunapatikana Tabata kimanga,jijini Dar es salaam".

Post a Comment

0 Comments