Ticker

6/recent/ticker-posts

VIJANA WATAKIWA KUTUMIA FURSA KUJIUNGA NA CHUO CHA ZIMAMOTO NA UOKOAJI

KUPITIA Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea, Chuo cha Mafunzo ya Uokoaji kimewakaribisha wananchi wenye sifa stahiki kujiunga na Chuo hicho kwani kinatoa kozi ndefu na kozi fupi,ambapo kozi ndefu inaanzia mwaka mmoja hadi miaka miwili na kozi fupi siku tatu hadi wiki mbili.

Akizungumza katika Maonesho hayo Mkufunzi wa chuo hicho Bi.Faraja John amesema chuo kinatoa fursa kwa wanafunzi wenye kazi au ajira kupata nafasi kwa masomo ya jioni.


" Sifa za kujiunga walau ufaulu wa masomo manne na moja ikiwa la sayansi,ada zetu ni nafuu na zinalipwa kwa awamu. Chuo kipo maeneo ya Ilala mkabala na Kituo cha Mwendokasi FIRE "amesema


Amesema jinsi ya kujiunga fomu inapatikana kwenye tovuti ya Chuo Cha Zimamoto na Uokoaji,au kwa watakao tembelea Banda la Jeshi la zima moto na uokoaji kwa watakaohitaji kujiunga,watasajiriwa.

Post a Comment

0 Comments