Ticker

6/recent/ticker-posts

JUMUIYA YA WAZAZI TANGA YAUNGA MKONO SERA YA RAIS DKT SAMIA YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga wa pili kutoka kulia akiwa ameshikilia mti mara baada ya kuzindua kampeni ya tembea na kivuli na kuimarisha lishe kwenye shule za Mkoa wa Tanga iliyokuwa ikiendeshwa na Taasisi ya Tanzania Environmental Agro Smart(T.E.A). wa kwanza kulia ni Katibu wa Wazazi wilaya ya Tanga Urassa Moses Nanyaro na kushoto Mjumbe wa Baraza la Wazazi wilaya ya Tanga Pamela Chaula.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga katikati akiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni hiyo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga akipanda mti mara baada ya kuzindua kampeni hiyo

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM wilaya ya Tanga Hamza Bwanga akipanda mti mara baada ya kuzindua kampeni hiyo

shughuli za usafi ikiendelea kwenye uwanja wa Lamore Jijini Tanga
usafi ukiendelea
Katribu wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Urassa Moses Nanyaro kulia akiwa na Katibu wa UVCCM wilaya ya Tanga wakifanya usafi
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Hamza Bwanga kulia akiwa na Katibu wa Jumuiya hiyo wilaya ya Tanga Urassa Moses Nanyaro na Mjumbe wa Jumuiya hiyo Pamela Chaula mara baada ya kumalizika kampeni ya upandaji wa miti
 

Na Oscar Assenga, TANGA.

JUMUIYA ya Wazazi wilaya ya Tanga imesema kwamba wataendelea kuunga mkono sera ya Rais Dkt Samia Suluhu ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira kwa kushirikiana na taasisi ambazo zinajihusisha na kampeni hizo ili kuleta manufaa kwa jamii.

Sambamba na hilo wataendelea kuhamasisha upandaji wa miti ya matunda katika maeneo mbalimbali ya Tanga ikiwa ni mkakati wa kuhakikisha mazingira yanatunzwa na baadae kuleta faida.

Hayo yalisemwa leo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga Hamza Bwanga wakati akizungumza mara baada ya kuzindua kampeni ya tembea na kivuli na kuimarisha lishe kwenye shule za Mkoa wa Tanga iliyokuwa ikiendeshwa na Taasisi ya Tanzania Environmental Agro Smart(T.E.A).

Alisema kwamba jambo la mazingira ni muhimu sana na moja ya jukumu lao kusimamia na wapo tayari muda wowote kushirikiana na taasisi ambazo zinatunza mazingira kwa kuleta manufaa.

“Niwapongeze Taasisi ya TEA mlilolifanya hapa ni jambo nzuri niwaombe tuendelea kuhirikiana nanyi kuhakikisha mazingira yetu yanaendelea kuwa mazuri”Alisema Mwenyekiti huyo.

Aidha alisema kwamba wataendelea kusimamia suala la utunzaji wa mazingira ikiwemo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa kuonyesha wanaunga mkono sera hiyo ambayo itasaidia kuzibiti uharibifu wake.

“Lakini niwaambie kwamba TEA mmetuwahi sisi tulishapanga na kuweka kwenye mipango yetu suala la uhamasishaji wa jamii kupanda miti katika maeneo mbalimbali katika wilaya ya Tanga “Alisema

Alisema pia miti yenye matunda ina faidi kubwa sana kwa jamii kwani ikitumiwa vizuri inaweza kuwa chanzo cha wao kuweza kupata kipato lakini kuwapa afya bora.

Hata hivyo alisema kwamba wanahaidi kwamba hawatachoka wakati wowote watapokwenda mahali popote watakuwa wakitoa ushauri juu ya kampeni ya tembea na kivuli kuhakikisha mazingira yanakuwa mazuri.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Tanga wapo vizuri chini ya CCM huku akimpongeza Diwani wa Kata ya Majengo kwa kuunga mkono jambo hilo akiwa pamoja na Mwenyekiti wa CCM kata ya Majengo.

Katika hatua nyengine Mwenyekiti huyo alisema kwamba wataendelea kushirikiana kwenye kampeni hiyo kuelimisha ili jamii iweze kuwa na uelewa mzuri wa upandaji wa miti hususani ya matunda na kivuli.

Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Afisa Mazingira Mkoa wa Tanga Sosiya – aliishukuru Shirika la TEA kuichangua Jiji la Tanga kwenye kampeni hiyo ya uzinduzi ambayo ina umuhimu mkubwa .

Alisema kwani hilo jambo ni maagizo ya kisera na kanuni kila Halmashauri nchini inatakiwa kupanda miti isiyopungua milioni 1.5 kila mwaka na kwa takwimu hadi mwezi Mei 30 mwaka huu mkoa wa Tanga wamefanikiwa kupanda zaidi ya miti milioni 11 kat iya miti milioni 16.5 .

“Leo tunayofuraha kwamba Shirika la TEA limekuja kutushika mkono katika utekeleza kampeni hiyo kwa asilimia 100 hivyo viongozi a wananchi wakiande kuupokea mradi huo kwani utakuwa na manufaa makubwa sana “Alisema

Katibu wa Wazazi wilaya ya Tanga Urassa alilipongeza Shirika l;a TEA kwa jambo hilo ambalo wamelifanya huku akieleza kwamba CCM ndio iliyopewa dhamana kwenye ilani ya Uchaguzi 2020/2025 kusimamia eneo la elimu na mazingira .

Alisema kwamba wanapoona wanaungwa mkono kwenye utekelezaji wa ilani ya CCM kuhusu mazingira wanafarijika huku akiwapongeza viongozi wa Kata ya Majengo kwa kulisimamia zoezi hilo ipasavyo.

Post a Comment

0 Comments