Ticker

6/recent/ticker-posts

MKURUGENZI DCEA ATEMBELEA BANDA LA DCEA SABASABA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya imeendelea kutoa elimu kwa wananchi kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar es Salaam juu ya athari ya za dawa za kulevya na sheria zinazoongoza Mamlaka pamoja na zinazoongoza kwa wale wanaokamatwa na dawa za kulevya.

Akizungumza katika Maonesho hayo leo Julai 5,2023 Jijini Dar es Salaam, Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Aretas Lyimo amesema ni muhimu wananchi wakawa na uelewa wa kutosha ili kuhakikisha na wao wanakuwa mabalozi wazuri kwaajili ya kuelimisha wenzao kujiepusha na dawa za kulevy.a

Amesema Dawa za kulevya zina athari kubwa kwa wananchi ikiwemo kuharibu uchumi wetu pamoja na kuharibu mnyororo mzima wauchumi wa nchi kwasababu nguvu kazi ya vijana ambao ni wajenzi wa taifa wanaathirika kwa kuangukia kwenye matumizi ya dawa hizo.

"Sasa hivi wanafunzi waliowengi wa shule za msingi, sekondari na vyuo ndio wanaangukia kwenye matumizi ya dawa za kulevya, tunajikuta tunaharibu taifa letu kwa kutokuwa na watu ambao wanaelimu ya kutosha kwasababu wengi wanaishia bila kumalizia shulezao kutokana na kutumia dawa za kulevya". Amesema

Aidha amewaasa wananchi kwa ujumla kusaidia wanaelimisha watu wengine kuhakikisha kwamba wanaepukana na dawa za kulevya ili taifa liendelee kuwa salama dhidi ya athari za matumizi ya dawa za kulevya.

Pamoja na hayo amesema kuwa Mamlaka imejipanga vizuri kuhakikisha kwamba wanatokomeza tatizo la dawa za kulevya nchini ili kuweza kujenga uchumi wetu imara na watafanya operesheni mbalimbali nchi nzima na kutoa elimu kwa jamii ili iweze kuwa na uelewa mpana kuhusu athari za matumizi ya dawa za kulevya

Hata hivyo Kamishna Jenerali Lyimo alitembelea mabanda mengine ya wadau ambao mara nyingi wamekuwa wakishirikiana nao katika kuhakikisha wanadhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini, wakiwemo wadau wao TAKUKURU, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali pamoja na wadau wengine ambao wameshiriki kwenye Maonesho hayo.
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Aretas Lyimo akizungumza na watumishi wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba leo Julai 5,2023 Jijini Dar es Salaam
Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Aretas Lyimo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea banda la Mamlaka hiyo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba leo Julai 5,2023 Jijini Dar es Salaam



Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya. Aretas Lyimo akitembelea mabanda ya wadau mbalimbali ambao wamekuwa wakishirikkiana katika kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya nchini, katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba leo Julai 5,2023 Jijini Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments