Ticker

6/recent/ticker-posts

RC CHALAMILA AFUNGUA BONANZA LA MICHEZO TRA KARIAKOO NA WAFANYABIASHARA

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Albert Chalamila amefungua na kukabidhi zawadi kwa washindi kwenye Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza kwenye Bonanza hilo leo Julai 1,2023 Mhe.Chalamila ameipongeza TRA pamoja na Wanyabiashara kwa kuweza kukutana pamoja na kuandaa Bonanza hilo ambalo limekuwa na umuhimu mkubwa wa kuwaweka pamoja na kati ya wafanyabiashara ambao ni walipa kodi pamoja na TRA ambao ni wakusanyaji wa kodi.

Aidha Mhe.Chalamila aimeitaka Mamlaka ya Mapato nchini(TRA) kuhakikisha wanabuni njia nzuri zaidi ambayo itatumika katika ukusanyaji kodi kwa wafanyabiashara kwani itasaidia kupunguza manung'uniko kwa wafanyabiashara.

"Nawaomba muwe wabunifu,fanyeni kama mlivyotoa kodi ya Road licence mkaitoa na kuiweka kwenye mafuta leo hakuna mfanyabiashara au mtanzania anayelalamika mnatakiwa kufanya kama hivi"Amesema Chalamila.

Hata hivyo,Chalamila amewakata watanzania kuwa juhudi katika kulh'pa kodi kwani kodi inayolipwa ndio inapelekea serikali kuendeleza miradi mbalimbali ya kimkakati huku akiwataka wafanyabiashara kutoichukulia TRA kama chombo cha unyang'anyi bali ni chombo chenye nia njema.

Pamoja na hayo Chalamila,amewatia moyo watendaji wa TRA kwa kuwasihi kufanya kazi kwa waredi na huku akisema hakuna mahali TRA inawezapendwa kupendwa kutokana na kazi inayofanya.

Kwa upande wake Kamishna Mkuu wa TRA, Bw.Alphayo Kidata, amesema wameamua kuanzisha Bonaza hilo hili kuweze kuweka uhusiano mzuri kati ya walipa kodi na wananchi.

Amesema kwa sasa mapato yameongezeka katika mkoa wa kikodi Kariakoo toka makusanyo ya Bilion 3 kwa mwezi mpaka bilioni 14 kwa mwezi baada ya kuanzishwa kwa huduma ya kikodi mkoa wa Kariakoo.


Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Albert Chalamila akikabidhi zawadi Kombe kwa washindi Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Albert Chalamila akikabidhi zawadi kwa washindi Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Albert Chalamila akizungumza katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA, Bw.Alphayo Kidata akizungumza katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Kamishna Kodi za Ndani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bw. Herbert Kabyemela akizungumza katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Wafanyabiashara akijaribu kupeleka mashambulizi kwa wapinzani wao TRA Kariakoo katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Mchezaji wa timu ya mpira wa miguu ya TRA Kariakoo akimiliki mpira katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Wanamichezo wakiwa kwenye Mchezo wa kukimbia na magunia katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Wanamichezo wakiwa kwenye Mchezo wa kukimbiza kuku katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.Wanamichezo wakiwa kwenye Mchezo wa kvuta kamba katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.
Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Albert Chalamila akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa TRA Kariakoo katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.


Mkoa wa Dar es salaam, Mhe.Albert Chalamila akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Wafanyabiashara katika Bonanza la Michezo TRA Kariakoo na Wafanyabiashara liliofanyika leo Julai 1,2023 katika viwanja vya JK Park Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Post a Comment

0 Comments