Ticker

6/recent/ticker-posts

RC MNDEME AZINDUA RASMI UZALISHAJI KATIKA MGODI WA ALMASI MWADUI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifungua mtambo wa kufungua na kufunga njia ya kumwaga maji tope katika bwawa jipya la tope laini ya mgodini wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Jumatatu Julai 17,2023. Kushoto ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwasha mitambo wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Jumatatu Julai 17,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifungua mtambo wa kufungua na kufunga njia ya kumwaga maji tope katika bwawa jipya la tope laini ya mgodini wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog 
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amezindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa uchimbaji madini ya Almasi (Williamson Diamond Limited) uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga ikiwa ni takribani miezi nane tangu mgodi huo usitishe uzalishaji baada ya kingo za Bwawa la Maji Tope kubomoka.

Novemba 7,2022 Bwawa la tope la mgodini katika mgodi wa Mwadui lilipasuka na kuharibu makazi na mashamba ya wananchi wa vijiji vya Ng'wanholo na Nyenze vilivyopo katika Kata ya Mwadui Luhumbo wilayani Kishapu kwa kufunikwa na tope.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo leo Jumatatu Julai 17,2023 Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme ameupongeza Mgodi huo kwa kuchukua hatua mbalimbali baada ya kingo za Bwawa la Maji Tope kubomoka na kusababisha athari kwenye vijiji vinavyozunguka mgodi.

Uzinduzi huo umefanyika siku chache baada ya Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko kuagiza mgodi wa Williamson Diamond Limited uanze shughuli za Uzalishaji kuanzia Julai 15 baada ya kuridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa.

“Nimezindua rasmi uzalishaji katika mgodi huu. Hongereni kwa hatua hii na kazi iendelee. Naomba shughuli za uzalishaji zifanyike kwa kasi(spidi nzuri) kwa viwango vinavyotakiwa ili tuweze kufidia muda tuliokuwa tumesimama, serikali ipate mapato, ajira ziendelee, halmashauri zipate mapato, miradi ya CSR iendelee na watu wote waliokuwa wanatoa huduma hapa mgodini waendelee na kazi”,amesema Mhe. Mndeme.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

“Tumejenga bwawa hili lakini tunatakiwa tuanze kujenga bwawa la akiba ili kuepuka kusimamisha shughuli za uzalishaji endapo patatokea tatizo. Lakini pia hakikisheni mnafuatilia bwawa hili jipya mkibaini kuna changamoto hatua za haraka zichukuliwe kuepuka athari zinazoweza kujitokeza”,ameongeza Mndeme.

Aidha amesema serikali itaendelea kushirikiana na mgodi huo katika masuala mbalimbali na kama kuna changamoto inajitokeza wasisite kuwasiliana na serikali huku akihamasisha mgodi huo kutunza mazingira.

Kwa upande wake, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda ameishukuru serikali kwa ushirikiano na msaada mkubwa iliotoa mpaka kufikia mgodi huo unaanza shughuli za uzalishaji.

“Tumekamilisha matengenezo ya bwawa la tope laini la mgodini kwa muda mfupi. Tulisimamisha uzalishaji kwa muda wa miezi nane, sasa tumerejesha mitambo yetu”,amesema Mhandisi Mwenda.

“Kwa muda tuliosimamisha shughuli za uzalishaji sisi mgodi tumepata hasara, serikali imepata hasara na wananchi wamepata hasara. Tutahakikisha uzalishaji unarudi kwenye viwango vile tulivyokuwa navyo kabla ya bwawa kupasuka”,ameongeza Mhandisi Mwenda.
Muonekano wa sehemu ya bwawa jipya la tope laini kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited

Naye Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kizalendo inayomilikiwa Watanzania ya City Engineering amesema bwawa hilo jipya walilolijenga ni imara na wamefuata taratibu zote zinazotakiwa na tayari wametoa mafunzo kwa wafanyakazi mgodini namna ya kutunza bwawa hilo.

Mbunge wa Jimbo la Kishapu Mhe. Boniphace Butondo na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Mhe. William Jijimya wameeleza kufurahishwa na habari njema ya kuanza shughuli za uzalishaji kwenye mgodi huo wakisema sasa miradi ya maendeleo kupitia fedha za CSR itaendelea, wananchi wapata ajira na serikali itapata mapato.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwasha mitambo wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Jumatatu Julai 17,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwasha mitambo wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Jumatatu Julai 17,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifungua mtambo wa kufungua na kufunga njia ya kumwaga maji tope katika bwawa jipya la tope laini ya mgodini wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga leo Jumatatu Julai 17,2023.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akifungua mtambo wa kufungua na kufunga njia ya kumwaga maji tope katika bwawa jipya la tope laini ya mgodini wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa kwanza kulia) kuhusu bwawa jipya la tope laini ya mgodini kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (katikati) akiangalia bwawa jipya la tope laini ya mgodini kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga, kulia kwake ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda, wa kwanza kulia ni Mbunge wa Kishapu, Mhe. Boniphace Butondo.
Mhandisi Mwelekezi wa Mradi wa Ujenzi wa bwawa la tope katika mgodi wa Williamson Diamond Limited, Mhandisi Anael Macha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kizalendo inayomilikiwa Watanzania ya City Engineering akielezea uimara wa bwawa jipya la tope laini katika Mgodi wa Williamson Diamond Limited.
Muonekano wa sehemu ya bwawa jipya la tope laini kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea na kumuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kushoto) eneo la Uchimbaji Madini ya Almasi katika mgodi wa Williamson Diamond Limited
Muonekano sehemu ya eneo la Uchimbaji Madini ya Almasi katika mgodi wa Williamson Diamond Limited
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea na kumuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kushoto) eneo la Uchimbaji Madini ya Almasi katika mgodi wa Williamson Diamond Limited
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea na kumuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kushoto) eneo la Uchimbaji Madini ya Almasi katika mgodi wa Williamson Diamond Limited
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akimwelezea na kumuonesha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (kushoto) eneo la Uchimbaji Madini ya Almasi katika mgodi wa Williamson Diamond Limited
Mbunge wa Kishapu Mhe. Boniphace Butondo akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mhe. William Jijimya akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizindua rasmi shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Williamson Diamond Ltd, Mhandisi Ayoub Abel Mwenda (kushoto) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme baada uzinduzi rasmi wa shughuli za uzalishaji kwenye Mgodi wa Williamson Diamond Limited uliopo Kishapu Mkoani Shinyanga

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Post a Comment

0 Comments