Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAVITUO VYA TAARIFA NA MAARIFA DAR ES SALAAM WAPATIWA ELIMU YA UTENGENEZAJI MBOJI

NA EMMANUEL MBATILO

WANAVITUO vya Taarifa na Maarifa vya Mkoa wa Dar es Salaam vinavyosimamiwa na Shirika la Mtandao wa Jinsia Tanzania TGNP, wametembelea eneo la Mkulima katika eneo la Mbezi Magufuli na kupata fursa kujifunza namna ya utengenezaji wa Mbolea (Mboji) kwaajili ya kilimo.

Akizungumza mara baada ya kupata elimu hiyo leo Julai 17,2023 Jijini Dar es Salaam, Mmoja wa Wanavituo vya Taarifa na Maarifa, Bw.Kondo Salumu amesema watahakikisha elimu ambayo wameipata kuipeleke kwenye jamii ili waweze kujikwamua kiuchumi kupitia Kilimo.

Amesema wamejifunza jinsi ya kutengeza mbolea (mboji) kwa njia rahisi ambayo kila mmoja mwenye kipato cha chini anaweza kutengeneza na kuweza kumsaidia kwenye Kilimo.

"Tumejufunza kuanzia hatua ya kwanza mpaka mwisho, na elimu hii ni bora kwetu kwani imetujengea uwezo wa kwenda kutengeneza mbolea ambayo kwa kiasi kikubwa inaenda kupunguza gharama ambazo tumekuwa tukitumia katika kununua mbolea". Amesema

Nae Rehema Josephat ambaye ni mwanakituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Majoye ameipongeza TGNP kwa kuwawezesha kufika katika maeneo mbalimbali kwaajili ya kujifunza masuala ya Kilimo na ufugaji biashara ambayo itawasaidia kuwaingizia kipato katika vituo vyao.


Post a Comment

0 Comments