Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI TABIA AKAGUA MATENGENEZO YA UWANJA WA AMANI

Na Khadija Khamis Maelezo ,11-07-2023.

Zaidi ya shilingi Billion 15 zitatumika kuufanyia matengenezo uwanja wa mpira wa Amani studium ambao ujenzi wake umeanza hivi karibuni .

Matengenezo hayo yatajumuisha ujenzi wa Hoteli, Ukumbi wa Judo,viwanja viwili vidogo vya mpira wa miguu, viwanja vya mpira wa mikono,mpira wa wavu masumbwi na vyenginevyo

Aliyasema hayo Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe,Tabia Maulid Mwita wakati alipotembea maeneo viwanja vya amani kuangalia ujenzi wa ukarabati wa viwanja hivyo vinavyoendelea hivi sasa .

Aidha alisema lengo la matengenezo hayo ni kuwa na kiwanja cha Mpira cha kisasa chenye hadhi ya kitaifa na kimataifa ambacho kitakuwa na uwanja mkubwa wa kuingia watu wengi zaidi.

Alifahamisha kuwa katika ujenzi huo kumezingatiwa watu wenye mahitaji maalum kwa kurahisishiwa huduma zote muhimu .

Aidha alisema kuwa matengenezo ya uwanja huo utajumuisha kuweka nyasi za kiwango cha kwanza, Tatan mpya na paa kwa wananchi wote kwa kuzuia jua na mvua .

Ameeleza kuwa hadi sasa matengenezo hayo yemefikia asilimia 25 ya ujenzi na inatarajiwa uwanja huo kuingiza watu zaidi ya elfu 15.

Amesema kutakuwa na mabango ya biashara ya kielectroniki ambayo Serikali itakuwa na ubia na wafanyabiashara mbali mbali kutangaza biashara zao .

Nae Meneja wa Ujenzi huo Ahmet Ugur Isler kutoka kampuni ya Orkun ya Uturuki amesema atahakikisha matengenezo hayo yanamalizika kwa mujibu wa mkataba uliowekwa kati yao na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Matengenezo ya ujenzi huo wa Amani studium inatekelezwa na Kampuni ya Orkun kutoka Nchini Uturukiambao unatarajiwa kumalizika kabla ya mwezi wa Disemba mwaka huu .
Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe Tabia Maulid Mwita akitembelea Uwanja wa Amani ambao umo katika matengenezo unaotarajiwa kukamilika disemba huko Amani Mkoa wa Mjini Unguja Picha na Rahima Mohamed Habari Maelezo Zanzibar.

Meneja wa ujenzi kutoka kampuni ya Orkun ya Uturuki Ahmet Ugor Isler akimuelezea Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe Tabia Maulid Mwita kuhusu hali inavyoendelea katika ukarabati hali ya uwanja huo na kumuhakikishia kukamilika kwa muda uliopangwa . Picha na Rahima Mohamed Habari Maelezo Zanzibar.

Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo Mhe Tabia Maulid Mwita akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ukarabati wa Uwanja huo kwa ajili ya kutumika katika shughuli mbalimbali. Picha na Rahima Mohamed Habari Maelezo Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments