Wizara ya Viwanda na Biashara imeendelea kutoa huduma kwa wadau na wananchi kwa ujumla katika Maonesho 47 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Katika Maonesho hayo ambayo yameanza Juni 28 na kutatajiwa kufikia tamati Julai 13,2023, Wizara imekuwa ikishirikiana na taasisi mbalimbali ambazo zipo chini ya Wizara hiyo katika kuhakikisha Wajasiriamali, wafanyabiashara wadogowadogo, wa kati na wakubwa wanapata huduma stahiki.
Watumishi Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakiwa tayari kuzungumza na wadau na Wananchi wanaotembelea banda la Wizara katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yaliyozinduliwa leo tarehe 05.07.2023
0 Comments