Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga Rajabu Abdalla akishauriana jambo Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Eliazary Rweikiza kushoto mbele ya Waziri Prof. Mbarawa.
Waziri Prof Mbarawa akisalimiana na viongozi wa Wilaya ya Pangani.
********
Na Hamida Kamchalla, PANGANI.
WAZIRI wa ujenzi Profesa Makame Mbarawa ameagiza wakala wa barabara TANROADS wa Tanga kuhakikisha wanamsimamia mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa daraja la Pangani ili liweze kukamilika kwa wakati kwakuwa serikali imewekeza fedha nyingi katika mradi huo unaotajwa kuchochea kasi ya uchumi.
Waziri Mbarawa ametoa kauli hiyo wakati alipotembelea mradi huo kwa lengo la kujionea maendeleo uliopofikia akiambatana na viongozi mbalimbali wa chama na serikali ambapo akiwa katika mradi huo alisisitiza Tanroads kushirikiana na mkandarasi huyo ili afanye kazi yake kwa ufanisi kwa kuwa mradi huo unakwenda kufungua Mkoa wa Tanga katika suala zima la uchumi.
"Daraja hili ni muhimu sana na ni daraja kubwa linalojengwa kwa urefu wa kilomita 525 ni maeneo machache nchini mwetu yenye madaraja marefu kama hili hivyo tushirikiane na mkandarasi ili afanye kazi yake kwa ufanisi na kwa wakati ambao tumekubaliana" amesisitiza Waziri Mbarawa.
"Niwaombe sana watu wa Tanroads nyinyi mnakuwepo hapa wakati wote lazima mumsimamie mkandarasi huyu aifanye kazi hii kwa uadilifu mkubwa kwa kuwa serikali imetoa fedha nyingi,
"Katika wilaya hii mheshimiwa Rais ameleta takribani bilioni 240 nimshukuru sana mheshiwa Rais kwa kupenda wananchi wa Pangani na kwa kuonyesha mapenzi makubwa kwa wana Pangani na kuweza kutoa fedha hizo ambapo hivi sasa kazi zinaendelea vizuri" amesema Profesa Mbarawa.
“Hatutaki kuona mkandarasi tunampa kazi analipwa fedha nyingi lakini anakwenda kuchukua vifaa vibovu nchi za jirani ambavyo vimekuwa havifanyi kazi tunataka tunapomlipa mkandarasi fedha alete vifaa vizuri na vyenye uwezo,
"Lakini pia tunataka alete wafanyakazi wazuri na wenye uwezo na tunataka pesa tunayomlipa hapa isitoke na kwenda kupelekwa sehemu nyingine tunataka itumike kwenye mradi husika" alisistiza Mbarawa.
Mwenyekiti wa Ccm Mkoa wa Tanga Rajabu Abdalla amesema kitendo cha serikali kupeleka mradi huo mkubwa katika Wilaya hiyo ni kurahisisha utekelezaji wa ilani ya chama kwa kuondoa vilio vya wananchi katika kumaliza tatizo la maji.
Aidha amesema kwa miradi mikubwa inayotekelezwa ikiwa ni pamoja na ya barabara itpelekea kufungua fursa za kiuchumi, siyo tu kwa Wilaya ya Pangani bali ni kwa Mkoa mzima wa Tanga.
"Kila sehemu kuna siasa zake, na kwa hapa Pangani siasa zetu ni kwenye suala zima la barabara hii ya Tanga- Pangani pamoja na maji, kwahiyo hili linalofanyika kwa sisi tunaogombea kupigiwa kura,
"Hii itachangia kwa sana kwenye chaguzi zijazo kutokutumia nguvu kubwa sana katika kuomba kura, kwa sababu wananchi wanaona kinachofanyika na wanamshukuru sana Mh.Rais" amesema.
0 Comments