Ticker

6/recent/ticker-posts

TUMIENI USHAIRI KUKEMEA MMOMONYOKO WA MAADILI – WAZIRI CHANA

Na Brown Jonas WUSM Dar Es Salaam

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana leo Agosti 12, 2023 Jijini Dar es Salaam amewahimiza washairi kutumia Sanaa hiyo kutunga mashairi yatakayosaidia kukemea mmomonyoko wa maadili nchini.

Mhe. Chana amesema hayo katika kilele cha Kongamano la tatu la Chama cha Usanifu wa Kiswahili na Ushairi Tanzania (UKUTA)

“Hivi karibuni, kumekuwa na wimbi kubwa la mmomonyoko wa maadili
hasa vijana na watoto kupuuza mila na desturi za kitanzania kwa kuiga tamaduni za kigeni. Ushairi ni mojawapo ya nyenzo ya kukemea vitendo vinavyokiuka maadili yetu na kuelimisha jamii kuthamini misingi ya utamaduni wetu.” amesema Dkt. Chana

Kongamano hilo limehudhuriwa na wadau mbalimbali wa Sanaa za ushariki kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ambapo kongamano la Nne limepangwa kufanyika Jijini Dodoma mapema mwakani.Post a Comment

0 Comments