Ticker

6/recent/ticker-posts

UWEKEZAJI WA BANDARI KUCHANGIA MAENDELEO KWA TAIFA-PINDA

Watanzania kutobeza fursa za Uwekezaji zilizopo Nchini ikiwemo Uwekezaji katika Bandari, kwani Uwekezaji huo utachangia katika kuleta maendeleo kwa Taifa.

Mhe. Pinda ametoa pongezi hizo tarehe 7 Agosti, 2023 alipotembelea banda la TPA katika Maonesho ya kitaifa ya Wakulima Nanenane 2023 yanayofanyika katika Viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya.

Aidha, Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Pinda ameshauri elimu zaidi iendelee kutolewa kwa Wananchi kuhusu Uwekezaji huo.

Mhe. Pinda pia ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa bandari Tanzania TPA, kwa Kushiriki Maonesho ya Kitaifa ya Wakulima NaneNane 2023 na kutoa Elimu kwa Umma kuhusu huduma zinazotolewa na Bandari.

Akimkaribisha Mhe. Waziri Mkuu Mstaafu kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa TPA Bw. Nicodemus Mushi, amesema Mamlaka hiyo inaendelea na mipango ya kuboresha Bandari Nchini zikiwemo Bandari za Maziwa, kwa lengo la kuboresha huduma na kuongeza ufanisi zaidi katika Bandari

Post a Comment

0 Comments