Ticker

6/recent/ticker-posts

WAKANDARASI WAONYWE WAKIKOSEA, WAKIADHIBIWA WASILALAMIKE.

Waziri Prof. Mbarawa akifanya ukaguzi katika kipande cha barabara.
Waziri akiongea na waandishi wa habari.
Waziri akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri wa kampuni ya Beza Consulting Engineers PLC Peter Dondo katikati kwenye eneo la barabara.

*************

SERIKALI imeshauri kwa Wahandisi Washauri kusimamia na kufuatilia kwa ukaribu Wakandarasi wanaotekeleza miradi mikubwa ili wanapofanya kinyume na mikataba iweze kuwabana na kuwapa adhabu inayostahili.


Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof Makame Mbarawa ametoa kauli hiyo wilayani Pangani alipotembelea kukagua barabara ya Tungamaa-Mkwaja hadi Mkange yenye urefu wa km 95.2 iliyogarimu zaidi ya sh bilioni 94 ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi machi, 31, 2025.


Alisema inapotokea Mkandarasi amekwenda kinyume na utekelezaji au akizembea, ni wajibu wa Mhandisi Mshauri kumpa onyo mara kwa mara ili aelewe makosa yake na inapotokea amepewa adhabu asione kama haikumstahili.


Prof Mbarawa amesema kuwa ujenzi wa mradi huo unasuasua huku Mkandarasi akiwa ameshalipwa kiasi kikubwa cha fedha lakini hajafikia hatua inayostahiki ikiwa ni pamoja na fedha kutumika na mradi kutokamilika.


"Mhandisi wewe ndiye unasimamia mradi hivyo nataka kila kitu unamuandikia, kwasababu hiyo itaisaidia TANROADS wakati wa kutoa maamuzi, kama ww Mshaurri hautaweka rekodi nzuri, wala hukumpa onyo kisha wakati wa maamuzi ikija adhabu ajue kwanini amepewa adhabu. amesisitiza Prof.


"Manendeleo ni mazuri lakini tuendelee kumbana Mkandarasi aende kwa wakati, kuna maeneo ambayo yamechellewa kwa asilimia 12, barabara hii inatakiwa kuisha machi 2025, sasa ikianza kunyesha mvua biashara yetu itakuwa imeishia pale" amesema.


Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Tanga Eliazary Rweikiza amesema mradi huo unatekelezwa kampuni ya Chona Railway 15 Bureau Group Corporation na kusimamiwa na kampuni ya Beza Consulting Engineers PLC ini JV with Cheil Engineering Co. Ltd mkataba wake ulitiwa saini mwezi Agosti 2021 na kuanza kazi mwezi April 2022.


Rweikiza amebainisha kwamba katika hatua za utekelezaji wa mradi kumekuwa na matatizo mbalimbali ikiwemo kucheleweshwa uhamishwaji wa miundombinu, ikiwemo mabomba ya maji safi, nguzo za umeme pamoja na nyaya za simu.


"Pia kulikuwa na wananchi ambao waliokataa kukubaliana na fidia za mali zao zilizoudhinishwa na Mthamini mkuu wa serikali, lakini pia mvua zilizonyesha mfululizo zilisababisha kasi ya ujenzi kupungu,


"Kuna baadhi ya wataalamu muhimu wa Mhandisi Mshauri kuondolea kwa kutotekwlwza majukumu yao pamoja na Mkandarasi kuwa na vifaa vichache vya ujenzi" amefafanua Rweikiza.


Aidha kutokana na matatizo hayo Rweikiza amemshauri Mkandarasi huyo kuongeza mitambo ya kufanyia kazi ili kuepuka kuchelewesha mradi kwani muda uliotumika na hatua iliyofikiwa siyo matarajio yao.


"Aanze maandalizi mapema maandalizi ya kuleta mitambo ya lami na kununua lami yenyewe na kuisaga kokoto zinazotumika lakini pia pesa wanazolipwa wazitumie kwenye mradi mradi huu na sio kupeleka kwenye miradi mingine wanayotekeleza" amesema.


"Lakini pia tunamshauri aanze kujenga matabaka juu ya barabara na ni matemeo yetu kuwa Mkandarasi kama akizingatia ushauri wetu huu kazi itakwenda vizuri na itakamilika kwa wakati" amebainisha Rweikiza.

Post a Comment

0 Comments