Ticker

6/recent/ticker-posts

Katibu CCM aipongeza shule ya East Africa Dodoma

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

MWENYEKITI wa Wazazi (CCM) Mkoa wa Morogoro, Dk. Rose Rwakatare, ameishukuru serikali kwa kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wazawa.

Alitoa shukrani hizo jana jijini Dodoma wakati wa mahafali ya kwanza ya darasa la saba shule ya Awali na Msingi ya East Africa ya mkoani Dodoma.

“Serikali ilipohamia hapa wakati wa hayati Rais Magufuli alitoa wito kwa wawekezaji kuwekeza miundombinu mbalimbali ili kusaidia kutoa elimu na sisi kama watua mabo tumebobea katika elimu tuliamua kuwekeza kwa kujenga shule hii ili kuweza kutoa elimu bora”alisema

Alisema lengo la shule ni kuunga mkono jitihada za serikali katika utoaji wa elimu bora kwa watoto wa kitanzania ili kuwawezesha kutoa ushindani katika soko la ajira duniani.

Alisema shule hiyo itaendelea kuwa shule bora kwa kuhakikisha inakuwa kwenye orodha za kuu kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa na kimkoa .

Naye Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, alisema kutokana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili wazazi wanatakiwa kuwalinda watoto ili wasiharibiwe na tamaduni za kigeni ikiwemo kujihusisha na vitendo vya ndoa za jinsia moja.

Mbaga, alisema hivi sasa Dunia imeharibika sana hivyo wazazi wanao wajibu wa kuhakikisha wanawalinda watoto wao ili wasiharibiwe na tamaduni za mataifa mengine.

“Hivi sasa ndugu zangu dunia imeharibika sana vitendo vya mmomonyoko wa maadili vimekithiri sana hivyo wazazi mnapaswa kuwalinda watoto ili wasiharibiwe na tamaduni za mataifa mengi.

“Mataifa ambayo yamekuwa yakihamasisha masuala ya ndoa za jinsia moja na mambo mengine ambayo ni kunyume ya tamaduni za kitanzania na nikinyume na mpango wa Mungu”alisema Mbaga

Aidha, aliwataka wazazi kuacha tabia ya kutelekeza suala la malezi ya watoto kwa walimu pekee yao bali wanapaswa kuwasimamia na kuwafuatilia kila wakati ili wabaini vikwazo ambayo wanakabiliwa navyo.

“Wazazi hatupaswi kuacha suala la malezi kwa walimu pekee yao bali tuhakikishe kuwa tunawafuatilia watoto wetu kwa kushirikiana na walimu ili kuwasaidia wasiingie kwenye mikono ya shetani hali ibadilika sana hivi sasa watoto wamekuwa na tabia za ajabu ambazo kama hatutakuwa makini nao tutawapoteza"alisema

Kadhalika, aliwataka walimu kuhakikisha kuwa wanasimamia watoto hasa wanapokuwa katika mabweni ili kubaini kama kuna mabadiliko yoyote ya kitabia na kuchukua hatua mapema kabla ya kundi kubwa kuharibiwa.

Vile vile, aliipongeza shule hiyo kwa kuunga mkono wa jitihada za serika katika uwekezaji kwenye sekta ya elimu ili kutoa elimu bora kwa watoto wa Kitanzania.

“Mkurugenzi niwapongeze sana kwa uwekezaji huu katika sekta ya elimu sisi chama pamoja na serikali kwa ujumla tutaendelea kutoa ushirikinao kwenu ili mfikie malengo yenu”alisema

Alisema azma ya serikali ya awamu ya sita ni kuboresha elimu ambapo hivi sasa imefanya uwekezaji mkubwa katika ujenzi wa madarasa,maabara, mabweni pamoja na miundombinu mingine ili kuinua kiwango cha elimu nchini.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akizungumza kwenye mahafali ya shule ya Awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wahitimu wa shule ya awali na Msingi ya East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma wakiwa kwenye mahafali yao yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa shule ya awali na msingi East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Dodoma Pilly Mbaga, akikabidhi cheti kwa mmoja wa wahitimu wa shule ya awali na msingi East Africa iliyoko Kikuyu Dodoma mwishoni mwa wiki
Mkurugenzi wa shule za St Marys na East Africa ya Kikuyu Dodoma, Dk. Rose Lwakatare akizungumza kwenye mahafali ya shule ya awani na msingi East Africa Dodoma yaliyofanyika mwishoni mwa wiki shuleni hapo


Post a Comment

0 Comments