Ticker

6/recent/ticker-posts

MAHAFALI YA 14 KATIKA SHULE YA SEKONDARI BUGANDIKA YAFANA ,WAZAZI WAASWA KUCHANGIA HUDUMA ZA KIJAMII.


Na Shemsa Mussa, Kagera.


Mahafali ya 14 katika shule ya sekondari Bugandika yafana ,huku wazazi na walezi wakihaswa kuchangia huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma ya chakula shuleni, na kuchangia miundombinu mingine huku serikali ikianzia wanapo ishia.

Akizungumza katika Mahafali hayo Afisa elimu kata Bugandika Wilaya Missenyi, Mwalimu MarryStella Stephano Kankiza amewataka wazazi na walezi katani humo, kuelekeza nguvu zao nyingi katika suala la lishe kwa watoto wao kwa kuchangia chakula shuleni ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi na hivyo kumjenga mtoto kimwili na kiakili.

“ifikapo mwezi Januari mwakani, nawasisitiza na kuwasihi wazazi, hakikisheni kila mtoto anapata chakula shuleni hili sio mwongozi wetu sisi ni agizo la serikali kwamba kila mtoto anatakiwa kupata chakula shuleni mfano mzuri tu nyie mmekuja asubuhi hapa ila najua njaa imeshawauma sana basi wahurumie wanaokuja saa 12 asubuhi na kuondoka saa 10 jioni "amesema MarryStella.

Aidha amewasihi wahitimu wa kidato cha nne kuyatengeneza maisha bora siku ya kufanya mtihani kwani siku hiyo ni siku maalum ya kuchagua ni maisha yapi unapenda kuyaishi na kuwakata kuzitumia siku zilizobaki kubadilika na kutengeneza maisha bora ya baadae .

"Yaani nyie wanangu kujilemba na kupendeza hivi haina maana sana kama matokeo yako yatakuja vibaya na utashindwa mtihani,leo kuna wazazi wamewabebea keki,chakula kizuri na maua hii ni kuonesha kuwa wanafuraha na wanawategemea sasa siku ya matokeo basi wafurahishe wazazi wenu zaidi ,shule zipo za kutosha mtasoma" ameongeza MarryStella.


Awali akisoma lisala kwa mgeni rasmi, mkuu wa shule ya sekondari ya Bugandika mwalimu Jesse Ndyakowa amesema shule hiyo licha ya mafanikio, inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo upungufu wa bweni la kulala la wanafunzi, ukosefu wa mashine ya kudurusu mitihani, kompiuta mbili, majengo mawili ya utawala na upungufu wa umeme.

“mheshimiwa mgeni rasimi licha ya mafanikio kadhaa ya shule yetu, lakini pia shule yetu inakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo tuna upungufu wa bweni la kulala la wanafunzi wanaotoka mbali hususani wasichana ili kupunguza uwezekano wa vishawishi njiani, tuna ukosefu wa mashine ya kudurusu mitihani kwani iliyopo ni mbovu na haifanyi kazi, tuna ukosefu wa kompiuta mbili kwa ajili ya kuchapa mitihani, tuna ukosefu wa majengo mawili ya utawala moja ikiwemo ofisi ya mwalimu mkuu ambapo mkuu wa shule ulazimika kutumia chumba cha mahabara ya fizikia na walimu kutumia vyumba vya madarasa kama mahabara na pia tuna upungufu wa umeme kwani haujafika katika vyumba vyote”amesema mwalimu Jesse.

Mpaka sasa wadau wa maendeleo wa kata ya Bugandika wamechangia tripu 19 za mawe kwa ajili ya kuanza ujenzi wa bweni jipya la kulala wanafunzi hasa wa kike kutokana na kutembea umbali mrefu kufika shuleni hapo ,katika mahafali hayo kumefanyika harambee ya uchangiaji wa mashine ya kudurusu mitihani na ununuzi wa komputa ambapo kiasi cha shilingi 368,700 kimechangwa huku ahadi ikiwa ni shilingi 350, 000 jumla ni shilingi 718,700 kwa fedha zote

Akizungumza katika mahafari ya 16 ya shule hiyo Steven Kamugisha Ndyakowa katibu wa mbunge wa jimbo la Nkenge Mhe.Flolence Kyombo aliyekuwa amealikwa kama mgeni rasmi katika mahafari hayo, amesema kuwa katika kuunga mkono juhudi za wadau katika ujenzi wa bweni hilo ofisi ya mbunge huyo itachangia shilingi milioni 2.

“niahidi hapa katika kuunga mkono juhudi za wadau kama group la whatsApp la Bugandika mpya ofisi ya mbunge italeta hapa shilingi milioni mbili ili kuhakikisha bweni ili linakamilika na watoto wetu wapate sehemu ya kulala” amesema bw. Ndyakowa.

Aidha katika kuhakikisha ukamilishaji wa ujenzi wa bweni hilo Bw. Ndyakowa ametaka kufanyike harambee ya uchangiaji wa bweni hilo tarehe 26 mwezi wa 12 mwaka huu ambapo pia ameahidi kuwa mbunge wa jimbo hilo atakuwepo kuwaunga mkono.

“niseme hatutakaa hapa kila siku tunaomba omba wakati tunauwezo wa kuchangia sisi wenyewe, sasa natoa maelekezo tarehe 26 mwezi wa 12 kufanyike harambee hapa ili tupate fedha ya kujenga bweni na uwezo huo tunao, sasa mwenyekiti wa shule, mkuu wa shule, watendaji kaa fikiria namna ya kufanya harambee hiyo tuwe na hosteli mahali hapa hatuwezi kukaa na maneneo maneno” ameongeza katibu huyo wa mbunge.

Pia katika hatua nyingine amewasisitiza wazazi na walezi, malezi bora kwa watato wao na kuwachangia chakula shuleni ili kuboresha lishe yao na kuwawezesha kufanya vizuri katika masomo yao na pia amewataka wanafunzi waliohitimu kusoma kwa bidii na kujiandaa na mtihani wao wa mwisho unaotarajiwa kufanyika tarehe 13 mwezi wa kumi na moja mwaka huu.


Jumla ya wanafunzi 100 wamehitimu katika shule hiyo ambapo wavulana ni 54 na wasichana ni 46.

Post a Comment

0 Comments