Ticker

6/recent/ticker-posts

NMB,YATOA MSAADA KATIKA SHULE ZA MISNGI NA SEKONDARI KWENYE HITIMISHO LA JUMA LA HUDUMA KWA WATEJA.


Na Shemsa Mussa ,Kagera.


Bank ya NMB imetoa msaada wa Viti ,meza ,Madawati na vifaa vya ujenzi katika shule za msingi na sekondari vyenye jumla ya thamani ya shiling Milioni 62 Katika Halmashauri mbili za Mkoa wa Kagera.

Akitoa taarifa katika hafla fupi ya makabidhiano na upokeaji wa Msaada huo iliyofanyika katika uwanja wa shule ya sekondari Rwamishenye Bw William Makoresho Mkuu wa idara ya taasisi ya serikali na binafsi kutoka NMB taifa amesema , katika kuhitimisha juma (week) ya huduma kwa wateja hapa kagera wameweza kutoa msaada katika jumla ya shule 9.


Amesema wametoa Madawati 50 katika shule ya Msingi Mubembe yenye thamani ya shilingi Milioni 5 na laki 5 ,Madawati 50 katika shule ya Msingi kikagati yenye thamani ya Milioni 5 na laki 5 ,Madawati 50 shule ya Msingi kibeta yenye thamani ya shilingi Milioni 5 na laki 5 ,Madawati 50 shule ya Msingi Itahawa yenye thamani ya shilingi Milioni 5 na laki 5 pamoja na Mabati na vifaa vingine vya kuezeka vyenye thamani ya Milioni 3 na laki 4


Aidha Bw Makoresho amesema wametoa viti 100 na meza 100 katika shule ya sekondari ya Samia suluhu vyenye thamani ya shilingi Milioni 10 na laki 7 ,viti 100 na meza 100 katika shule ya sekondeari Rukoma yenye thamani ya shilingi Milioni 10 na laki 8 ,viti 100 na meza 100 katika shule ya sekonsari Rwamishenye vyenye thamani ya shilingi Milioni 10 na laki 7 ,viti 50 na meza 50 katika shule ya sekondari Hamgembe vyenye thamani ya shilingi Milioni 5 na laki 5 ikiwa vifaa vyote vimeghalimu kiasi cha shilingi Milioni 62.




Pia Makoresho ameongeza kuwa mpaka sasa NMB ina Matawi 230 Wakala zaidi ya 20000 pamoja na Mashine za kutolea fedha (ATM ) 780 nchi nzima pi amesema kwa sasa wamezindua mfumo wa jamii bondi ambao unatoa fursa kwa mtu binafsi hadi kwenye taasisi hivyo yeyote ananafasi ya kuwekeza .


Nae Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mhe Erasto Sima Mkuu wa Wilaya ya Bukoba ameagiza kila Mwalimu aliyepokea msaada huo kuhakikisha vifaa hivyo vinadumu na kutunza kila kitu kinachotolewa na wadau wa Elimu wanaoendelea kushirikiana na serikali huku akiwahakikishia wananchi kuendelea kuiamini na kuitumia bank ya NMB na kufurahia fulsa za mikopo zinazotolewa na bank hiyo

Post a Comment

0 Comments