Ticker

6/recent/ticker-posts

OSHA, HERI FOUNDATION WATOA MSAADA WA PADS KWA WANAFUNZI SHULE YA SEC.KAMBANGWA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAKALA wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA) kwa kushirikiana na Taasisi ya HERI ambayo inajihusisha na masuala ya Afya na Elimu, wametoa msaada wa taulo za kike (PADS) kwa wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Kambangwa iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Msaada huo umetolewa leo Oktoba 11,2023 katika Tamasha la kumtia moyo mtoto wa kike kujikita kwenye masomo ambalo liliandaliwa na HERI Foundation katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani.

Akizungumza katika tukio hilo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), Bi.Khadija Mwenda amewataka wanafunzi wa kike kuzingatia masomo yao shuleni kwa kuongza bidii na kuepuka vishawishi vinavyoweza kumsababishia kukwamishwa kwenye masomo.

Aidha Bi. Mwenda amesema watoto wa kike wajikite kwenye masomo na Serikali ipo tayari kuhakikisha mtoto wa kike anapata elimu iliyobora na kumuwezesha kutimiza malengo yake hasa kwa kumtengenezea mazingira wezeshi katika sekta ya elimu.

Amesema tumeshuhudia katika takwimu mtoto wa kike kila anapofikia ngazi fulani ya elimu, namba inapungua wanaoendelea kwenye ngazi inayofuata, hivyo juhudi za kuwapa moyo inahitajika ili waweze kufika mbali kwenye suala la elimu.

"Tumeona Rais Samia Suluhu Hassani ametunikiwa shahada huko nchini India na ameikabidhi kama zawadi kwa mtoto wa kike, lengo lake ni kumuinua mtoto wakike. Yote ni kuhakikisha Elimu inafika kwa jamii lakini tukimwangalia mtoto wa kike kwani anapitia changamoto nyingi". Amesema.

Kwa upande wa waandaaji wa Tamasha hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa HERI Foundation, Bi.Susan Ngole amesema katika sehemu ya kurudisha kwa jamii wameweza kuandaa tamasha la kuwaelimisha watoto wa kike na kuwapatia taulo za kike ili waweze kujistili wakiwa kwenye siku za hedhi kwani imekuwa ni changamoto kwa baadhi ya watoto wa kike.

Amesema lengo lao kubwa ni kuhakikisha mtoto wa kike asirudi nyuma, hivyo aweze kupata elimu bora ambayo itamuwezesha kutimiza malengo yake na kuwa msaada kwa jamii.

Nae Mwalimu Mkuu Shule ya Sekondari Kambangwa, Mwl. Angelina Mwakalukila amewapongeza OSHA pamoja na Taasisi ya HERI kwa kuweza kufika shuleni hapo na kuweza kuwatia moyo wanafunzi wa kike kuongeza juhudi kwenye masomo yao.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), Bi.Khadija Mwenda akiwa pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa HERI Foundation, Bi.Susan Ngole wakikabidhi taulo za kike kwa wanafunzi wa kike shule ya sekondari Kambangwa leo Oktoba 11,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), Bi.Khadija Mwenda akizungumza katika Tamasha la kuwatia Moyo wanafunzi wakike katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, Tamasha anmbalo limeandaliwa na HERI Foundation ambalo limefanyika Shule ya Sekondari Kambangwa leo Oktoba 11,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa HERI Foundation, Bi.Susan Ngole akizungumza katika Tamasha la kuwatia Moyo wanafunzi wakike katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, Tamasha anmbalo limeandaliwa na HERI Foundation ambalo limefanyika Shule ya Sekondari Kambangwa leo Oktoba 11,2023 Jijini Dar es Salaam

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), Bi.Khadija Mwenda akimkabidhi zawadi mtoto wa kike ambaye alitoa burudani ya kuimba wimbo wa kumpongeza Rais Samia katika harakati za kumkomboa mtoto wa kike kwenye elimu katikaTamasha la kuwatia Moyo wanafunzi wakike katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, Tamasha anmbalo limeandaliwa na HERI Foundation ambalo limefanyika Shule ya Sekondari Kambangwa leo Oktoba 11,2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa HERI Foundation, Bi.Susan Ngole (mwenye tshirt nyekundu) akiungana na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama Mahala pa Kazi (OSHA), Bi.Khadija Mwenda kumkabidhi zawadi mtoto wa kike ambaye alitoa burudani ya kuimba wimbo wa kumpongeza Rais Samia katika harakati za kumkomboa mtoto wa kike kwenye elimu katikaTamasha la kuwatia Moyo wanafunzi wakike katika kuadhimisha Siku ya Mtoto wa Kike Duniani, Tamasha anmbalo limeandaliwa na HERI Foundation ambalo limefanyika Shule ya Sekondari Kambangwa leo Oktoba 11,2023 Jijini Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments