Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DK.SAMIA AZIDI KUFUNGUA MIKOA KWA MTANDAO BARABARA

RAIS Dk.Samia Suluhu Hassan ameendelea kuifungua nchi kwa mtandao wa barabara ambapo amezindua daraja la Msingi lenye urefu wa mita 100 na barabara za maingilio zenye urefu wa Kilomita moja kwa kiwango cha lami ambapo Sh.bilioni 11.14 zimetumika.

Kukamilika kwa daraja hilo lililopo Barabara ya Mkoa ya Kitukutu – Gumanga – Nyahala (Sibiti) inayounganisha Mkoa wa Singida, Mwanza na Mara kupitia Daraja la Sibiti lenye urefu wa mita 82 na kilomita 25 kuunga daraja ni juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita za kuboresha na kuunganisha Barabara Kuu na za mikoa Nchi nzima.


Uzinduzi wa daraja hilo umefanyika leo Oktoba 16, 2023 ambapo Rais Dk.Samia amewataka wananchi wa Mkoa wa Singida kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuona faida ya daraja hilo lililopo kijiji cha Msingi wilaya ya Mkalama.


Imeelezwa kwamba barabara hiyo ni barabara muhimu kwani inaanzia barabara kuu ya Singida kwenda Nzega na inaunganisha barabara itakayojengwa kwa utaratibu wa EPC+F inayoanzia Karatu – Mbulu – Hydom – Sibiti – Lagalo – Maswa yenye urefu wa Kilometa 389 ambazo ni barabara muhimu kiuchumi na kijamii.




Awali akitoa taarifa ya Mradi huo Waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema maagizo ya Rais Samia ya kuweka taa katika madaraja hayo yanatekelezwa na tayari daraja la Msingi limewekwa taa na madaraja mengine yatawekwa taa mara baada ya Mkandarasi kukamilisha ujenzi.


Bashungwa amemshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha za miradi hiyo pamoja na miradi mingine aliyoelekeza itekelezwe kwani inazidi kuunganisha mikoa ya Kanda ya Ziwa, mikoa ya kati na kanda ya kaskazini na kueleza Rais ni mtu wa kazi na anatekeleza ahadi zake kwa vitendo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na
Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa wakati akikagua Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa wakati wakivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na viongozi mara baada ya kufungua Daraja la Msingi lililopo Wilayani Mkalama katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri wa Ujenzi Mhe. Innocent Bashungwa pamoja na viongozi wengine wakati akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023


Shamrashamra za mapokezi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kuwasili katika eneo la Mkutano wa hadhara pembezoni mwa Daraja la Msingi, Wilayani Mkalama katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023
Taswira ya Daraja la Msingi lenye urefu wa Mita 100, lililopo katika Kijiji cha Msingi, Mkalama Mkoani Singida. Daraja hilo limezinduliwa Rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan tarehe 16 Oktoba, 2023
Viongozi mbalimbali pamoja na Wananchi waliohudhuria tukio la ufunguzi wa Daraja la Msingi lililopo Mkalama Mkoani Singida tarehe 16 Oktoba, 2023






Post a Comment

0 Comments