Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS SAMIA AHUDHURIA SHEREHE ZA MIAKA 59 YA UHURU WA ZAMBIA JIJINI LUSAKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikaribishwa Ikulu ya Lusaka na Mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema Ikulu Jijini Lusaka kabla ya kwenda kuhudhuria Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema wakati wakielekea kwenye viwanja vya Ikulu kwa ajili ya kuhudhuria Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa nchi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2023.

Kikundi cha ngoma kutoka Lusaka kikitumbuiza katika Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa Taifa la Zambia katika viwanja vya Ikulu ya Nchi hiyo tarehe 24 Oktoba, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama kwa ajili ya heshima ya Wimbo wa Taifa katika Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa Zambia tarehe 24 Oktoba, 2023.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama na Mwenyeji wake Rais wa Zambia Mhe. Hakainde Hichilema pamoja na viongozi wengine wakati Wimbo wa Taifa wa Tanzania ukiimbwa katika Sherehe za miaka 59 ya Uhuru wa Zambia tarehe 24 Oktoba, 2023.


Post a Comment

0 Comments