Ticker

6/recent/ticker-posts

TAFITI MPYA KUIBUA UHALISIA KWENYE JAMII

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

CHUO Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Upande wa Utafiti, kimefungua semina ya Siku Tano yenye lengo la kufanya Mapinduzi kuondoa fikra ya ukoloni katika kufanya tafiti ili kupata matokeo chanya yanayo tokana na Uhuru wa Kifkra.

Akizungumza na Waandishi wa habari leo Oktoba 23,2023 Jijini Dar es Salaam, Kaimu Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam- Utafiti, Prof. Nelson Boniface amesema kupitia semina hiyo yenye kauli mbiu inayosema "Kuondoa Hali ya Ukoloni katika namna ya kufanya Tafiti" wanaangalia namna ambavyo tumekuwa na athari za mambo ya ukoloni kwenye jamii na jinsi wanavyofanya tafiti ambavyo yamewaathiri.

Nae Rasi wa Ndaki za Sayansi ya Jamii na Dini Prof.Christine Noe amesema wamekutana ili kuona ni namna gani sahihi ya kufanya tafiti ili kupata matokeo chanya kutokana na tafiti kulingana na mabadiliko ya Ulimwengu.

"Usipo badilisha mbinu ya kufanya tafiti utakuwa unafanya kwa namna ya zamani, lazima kila wakati kufikiri kufanya jambo kwa namna tofauti, tunataka kufanya mambo tofauti na zamani mambo yalivyo kuwepo tunaondoa ukoloni katika kufundisha namna ya kufikiri". Amesema

Amesema Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kina fedha za ndani kwa ajili ya kufanya tafiti ingawa hazitoshelezi hivyo kinapokua na uhitaji ufadhili wa vyanzo vya nje pesa zinakotoka, wasipangiwe namna ya kufikiri katika kufanya tafiti.

Kwa upande wake Mratibu wa Kituo Cha Sayansi ya Jamii( Society and religion center) Bw.Thomas Ndaluka amesema kuwa wanahitaji tafiti wanazo fanya ziendane na uhalisia kwenda kuboresha maisha ya jamii zinazoguswa na tafiti hizo na kubadili fikra ya jamii na fikra za wafanya utafiti.

"Hakuna mtu anaye miliki ufahamu au utatuzi wa matatizo tunakuja na mbinu ambazo tukifanya kwa Pamoja zitaleta suluhisho la jamii husika sisi Kama watafiti tunapo enda kijijini tusiende na majibu yetu tunapoenda kufanya tafiti kumbe tukishirikiana na jamii na sisi kwa Pamoja tukiungana tutapata suluhisho la matatizo yanayo ikumba jamii"Amesema

Semina ya mafunzo hayo itafanyika kwa siku Saba Kisha kufanya utafiti eneo la Bagamoyo ambalo lina athari za Ukoloni na inashirikisha Wanafunzi wa Shahada ya Uzamivu kutoka vyuo vikuu vitatu kutoka Sweden na Afrika Magharibi ambapo Kuna ushiriki wa chuo kutoka Mali na Burknafaso.

Post a Comment

0 Comments