Ticker

6/recent/ticker-posts

WADAU WA ELIMU YA UALIMU WAJADILI MAFANIKIO YA MRADI WA TESP NCHINI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KUPITIA Mradi wa Kuimarisha Mafunzo ya Ualimu kwenye Vyuo vya Ualimu vinavyomilikiwa na Serikali (TESP) ambao unafadhiriwa na Serikali ya Canada mpaka sasa umeshafanyika ukarabati wa Vyuo nane nchini na kujenga Chuo kipya cha Kabanga ambacho kilifunguliwa na Rais Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan hivi karibuni mkoani Kigoma.

Chuo hicho kimejengwa kuwa mfano wa namna ambavyo taasisi zetu mbalimbali zinaweza kujifunza namna ya kujenga kwa kuzingatia mazingira kwani kimejengwa kwa kutumia mbinu za uhifadhi wa mazingira ikiwemo ukusanyaji wa maji, kutumia biogesi pamoja na namna ya majengo yanavyopangwa.

Akizungumza leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam wakati akifungua Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Mradi wa TESP unahamasisha kuangalia masuala ya usawa wa Kijinsia kwani imesaidia kuandaa mkakati wa jinsia katika vyuo vya ualimu pamoja na utekelezaji wa mkakati huo ambao unatumika katika vyuo vya ualimu pamoja na taasisi zingine za Wizara ya Elimu.

"Wameendelea kutoa mafunzo kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu kuanzia mafunzo ya namna ya ufundishaji, mafunzo ya menejimenti na mafunzo ya jinsia, haya yote yamefanyika kupitia mradi huu". Amesema Prof.Nombo.

Aidha amesema kuwa Serikali ya Canada wamesaidia kuwekeza katika vifaa vya kujifunzia kufundishia, wamesaidia kununua vitabu , laptop, printers kwahiyo kupitia mradi huo sasa hivi wakufunzi katika vyuo vyetu vya ualimu wanaweza kufundisha kwa njia ya kidigitali .

Pamoja na hayo amesema Vyuo 15 vya ualimu vimeshaunganishwa na mkongo wa Taifa ambao unawasaidia kupata mtandao kwa urahisi na kuweza kuwarahisishia katika kufundishia na kupata mada za kuweza kufundisha.

Amesema kupitia kikao hicho wadau wataangalia namna ya kuendeleza masuala mazuri ambayo yamepatikana kutokana na mradi wa TESP katika mfumo wa elimu kwenye masuala ya ujenzi, jinsia na kufundisha kwa kutumia TEHAMA.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Serikali ya Canada Mhe.Helen Fytche amesema kwa kuamini katika ushirikiano na Wizara kupitia mipango inayolenga usaidizi wa kibajeti kama vile TESP, Canada itasaidia moja kwa moja vipaumbele vya Serikali juu ya elimu.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akizungumza wakati akifungua Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akizungumza wakati akifungua Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula, akizungumza katika ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula, akizungumza katika ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Serikali ya Canada Mhe.Helen Fytche akizungumza katika ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi wa Elimu ya Ualimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Bw. Huruma Mageni akizungumza katika ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo wakati akifungua Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini wakifuatilia Ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu uliofanyika leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akipata picha ya pamoja na Wadau wa Elimu ya Ualimu wakati wa Ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo akipata picha ya pamoja na Wadau wa Elimu ya Ualimu wakati wa Ufunguzi wa Kikao Cha Wadau wa Elimu ya Ualimu nchini leo Oktoba 30,2023 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments