Ticker

6/recent/ticker-posts

WANAUME KWA WANAWAKE WATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMA MAGONJWA YA SARATANI MBALIMBALI.


Wanaume na wanawake wametakiwa kujitokeza kupima magonjwa ya saratani mbalimbali ili kujiepusha na kujikinga ugonjwa huo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ufunguzi wa upimaji wa Saratani ulifanyika katika Hospitali ya Rufaa Bukoba ,Meneja wa Huduma za kinga ya Saratani kutoka Taasisi ya saratani ya Oceannroad Dkt Maghuha Stephano amesema leo Tarehe 31/10/ 2023 ni siku ya ufunguzi wa huduma ya upimaji wa saratani kwa akina mama na baba hospitalini hapo.


Aidha Dkt Maghuha amesema Kulingana na takwimu za mwaka jana kwa upande wa wanawake ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi umeonekana kuongezeka kwa kasi ukifuatia na saratani ya matiti huku ugonjwa wa saratani ya koo la chakula kuongezeka na kufuatia saratani ya tezi dume kwa wanaume .


Dkt Maghuha ameongeza kuwa kufika Kagera ni moja ya agizo la Rais Dkt Samia Suluhu Hasan la kuhakikisha Hospitali za kibingwa zinatembelea Hospitali zote za Rufaa ili kuweza kuwasaidia wananchi hasa wale wenye kipato cha chini ambao hawawezi kufika katika hospitali za kibingwa ili waweze kupata huduma za Saratani .


"Kama mnavyojua ugonjwa wa saratani huongezeka kwa sababu mbalimbali ,Kwa hali hiyo sisi kama Taasisi ya Oceanroad tumeona tufike katika Hospitali za Mikoa hususani katika maeneo yaliyopo mbali na Dar es salaam ambapo Taasisi yetu ipo kwa ajili ya huduma za saratani na tumekuja kwa kazi ya Uchunguzi na Ugunduzi wa saratani,amesema Dkt Maghuha"


Pia Dkt Maghuha amewatoa hofu wanawake na wanaume akisema kuwa ugonjwa wa saratani ukigundulika mapema unatibika hivyo wajitokeze kwa wingi ndani ya siku tatu kwa wale wote walio na dalili na wasio na dalili ili kuangalia afya zao juu ya ugongwa huo na kusema kuwa wameanza kwa kuchunguza saratani zenye wagonjwa wengi ikiwemo saratani ya Mlango wa kizazi ,Matiti,na tezi dume na kusema huduma zote zinafanyika bila malipo.


Hata hivyo amesema kwa wale wote watakaobainika kuwa na viashiria pamoja na mabadiliko ya awali ya saratani timu ya saratani kutoka Oceanroad ipo katika Hospitali hiyo ya Rufaa kutoa huduma katika Ngazi hiyo na zoezi hilo litadumu ndani ya siku tatu kuanzia Tarehe 31/10/2023 hadi 2/11/2023.


Nao baadhi ya akina mama waliojitokeza katika zoezi hilo akiwemo Joyce Mugayuki na Sarah Kamugisha wamemshukuru Rais Samia pamoja na Taasisi ya Oceanroad kwa kuwajali na kutambua umuhimu wao katika taifa mpaka kufikiwa na huduma hiyo ya saratani na kuwasihi wanaume pamoja na wanawake kwenda kupima na kupata elimu juu ya ugonjwa huo.

Post a Comment

0 Comments