Ticker

6/recent/ticker-posts

BANDARI QUEENS YAENDELEA KUTOA DOZI LIGI DARAJA LA PILI

Timu ya Netiboli ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania- TPA “ Bandari Queens “ imeendelea kutembeza vipigo kwa timu pinzani Katika Mashindano ya ligi daraja la pili Taifa yanayofanyika Mkoani Katavi, ikiandikisha rekodi ya kushinda Michezo 7 mfululizo hadi sasa.

Bandari Queens inayonolewa na Kocha Judith Ilunda imekuwa mwiba kwa Timu pinzani Katika Mashindano hayo ambapo imefunga jumla ya magoli 379 na kuwa Timu gumzo.

Meneja wa timu hiyo Fatma Mwinjaka anasema wanajivunia kikosi bora na maandalizi Kabambe waliyopewa na Menejimenti ya TPA kuelekea Mashindano haya hivyo imani yao ni kutwaa ubingwa na kupanga ligi daraja la kwanza Taifa.

Kikosi cha Bandari Qeens kina Nyota wakongwe na chipukizi, wakiongozwa na Mfungaji wao mkongwe Neema Mwahu , Mwenye umri wa miaka 58 pamoja na Nahodha wao Irene Mitava.

Post a Comment

0 Comments