Ticker

6/recent/ticker-posts

KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAIS ATETA NA MENEJA USIMAMIZI MIRADI WA SHIRIKA LA MAZINGIRA LA UMOJA WA MATAIFA

Na Mwandishi Wetu,

DODOMA.

22.11.2023

Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga amekutana na kufanya mazungumzo na Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) Dkt. Daniel Pouakouyou.

Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jumatano Novemba 22, 2023 viongozi hao wamejadili utekelezaji wa Mradi wa Urejeshaji wa Uoto wa Asili na Uhifadhi wa Bioanuai (SLR) na kufanya mapitio ya vipaumbele vya miradi mipya ya mazingira inayoandaliwa na Tanzania kwa kushirikiana na UNEP.

Dkt. Pouakouyou amesema UNEP itaendelea kuwa mshirika wa Tanzania katika ufadhili wa miradi ya mazingira ukiwemo mradi wa SLR unaotekelezwa katika Mikoa 5 nchini iliyopo katika Mabonde ya Mto Ruaha na Bonde la Ziwa Rukwa ikijumuisha wilaya za Iringa, Wanging’ombe, Mbarali, Mbeya, Sumbawanga, Tanganyika na Mpibwe.

Ameongeza kuwa lengo la ziara hiyo ni kuangalia vipaumbele vya miradi mipya ya mazingira inayofadhiliwa na UNEP na kuona maeneo mahsusi yanayohitaji ushirikiano wa karibu baina ya shirika hilo na Serikali ikiwemo upatikanaji wa fedha za utekelezaji wa miradi hiyo.

Tunashukuru ushirikiano tunaendelea kuupata kutoka kwa Serikali. UNEP itaendelea kufadhili miradi mipya ya mazingira ikiwemo mradi wa uhifadhi wa maeneo ya ardhi oevu katika mfumo ikolojia ya bonde la Mto Wami-Ruvu ambalo ni moja ya vyanzo vikuu cha maji kwa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na maeneo ya jirani” amesema Dkt. Poukouyou.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga amemueleza Dkt. Poukouyou dhamira na juhudi zinazoendelea kuchukuliwa na Serikali katika kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira na mabadiliko wa mazingira ikiwemo urejeshaji wa uoto wa asili katika maeneo mbalimbali ya nchi.

“Tunaishukuru UNEP kwa kuendelea kufadhili miradi ya mazingira hapa nchini. Tumeandaa Mpango Kabambe wa Mazingira wa mwaka 2022-2032 ambapo moja ya maeneo kipaumbele ni pamoja na urejeshaji wa uoto wa asili, bioanuai na kuboresha hali ya mifumo-ikolojia na kujenga uwezo wa jamii kuwa na shughuli endelevu za uzalishaji” amesema Bi. Maganga.

Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Wataalamu mbalimbali kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Ofisi akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Dkt. Paul Deogratius na Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa SLR, Dkt. Damas Mapunda na Afisa Mazingira Mwandamizi, Bw. Thomas Chali.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akiongoza kikao baina ya Watendaji Waandamizi wa Ofisi hiyo na Meneja Usimamizi Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyou. Kikao hicho kililenga katika kujadili utekelezaji wa Mradi wa urejeshaji wa uoto wa asili na kuhifadhi bioanuai (SLR) na vipaumbele vipya vya miradi ya mazingira nchini. Kikao hicho kimefanyika leo Jumatano Novemba 22, 2023.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akizungumza jambo na Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyou wakati wa kikao baina yao kilichofanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jumatano Novemba 22, 2023. Kikao hicho kililenga katika kujadili utekelezaji wa Mradi wa urejeshaji wa uoto wa asili na kuhifadhi bioanuai (SLR) na vipaumbele vipya vya miradi ya mazingira nchini
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akibadilishana mawazo na Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyou pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Dkt. Paul Deogratius muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao baina yao katika Ofisi za Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jumatano Novemba 22, 2023. Kikao hicho kililenga katika kujadili utekelezaji wa Mradi wa urejeshaji wa uoto wa asili na kuhifadhi bioanuai (SLR) na vipaumbele vipya vya miradi ya mazingira nchini
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akibadilishana mawazo na Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyou pamoja na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rail Dkt. Paul Deogratius muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi za Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jumatano Novemba 22, 2023.
Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyou akizungumza jambo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga na Watendaji waandamizi wa Ofisi hiyo muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Paul Deogratius na kushoto ni Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Urejeshaji wa Uoto wa Asili na Uhifadhi wa Bioanuai (SLR) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Damas Mapunda.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akiwa katika picha ya pamoja na Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyou muda mfupi baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jumatano Novemba 22, 2023. Kikao hicho kililenga katika kujadili utekelezaji wa Mradi wa urejeshaji wa uoto wa asili na kuhifadhi bioanuai (SLR) na vipaumbele vipya vya miradi ya mazingira nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akiagana na Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyoumuda mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi za Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jumatano Novemba 22, 2023. Kikao hicho kililenga katika kujadili utekelezaji wa Mradi wa urejeshaji wa uoto wa asili na kuhifadhi bioanuai (SLR) na vipaumbele vipya vya miradi ya mazingira nchini.
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akiagana na Meneja Usimamizi wa Miradi inayofadhiliwa na Mfuko wa Mazingira wa Dunia kutoka Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP), Dkt. Daniel Pouakouyou muda mara baada ya kumalizika kwa kikao baina yao kilichofanyika katika Ofisi za Mji wa Serikali, Mtumba Jijini Dodoma leo Jumatano Novemba 22, 2023. Wengine pichani ni Watendaji Waandamizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais akiwemo Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Dkt. Paul Deogratius (kulia) na kushoto ni Mratibu wa Kitaifa wa Mradi wa Urejeshaji wa Uoto wa Asili na Uhifadhi wa Bioanuai (SLR) kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Damas Mapunda. Kikao hicho kililenga katika kujadili utekelezaji wa Mradi wa urejeshaji wa uoto wa asili na kuhifadhi bioanuai (SLR) na vipaumbele vipya vya miradi ya mazingira nchini.


(NA MPIGAPICHA WETU)

Post a Comment

0 Comments