Ticker

6/recent/ticker-posts

SELF MICROFIANCE FUND YATOA MIKOPO YA BILLION 240 WATU ZAIDI YA LAKI MBILI WANUFAIKA



Meneja Masoko na Uhamasishaji Self Microfinance Fund Linda Mshana kupitia maonyesho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa yanayoendelea katika viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha yenye kauli mbiu elimu ya fedha, msingi wa maendeleo ya uchumi, amewaomba wananchi wote kupitia banda la Self Microfinance Fund kupata elimu ya mkopo.

Akizungumza na waandishi wa habari meneja masoko na uhamasishaji Linda amesema kuwa lengo la Self Microfinance fund katika maonyesho hayo ni kutoa elimu ya mikopo kwa mwananchi mmoja mmoja lakini pia hata kwa vikundi ili kuwaepusha na taasisi ambazo sio rasmi za kutoa mikopo ikiwemo mikopo ya kausha damu inayopelekea mkopaji kuchukuliwa kila kitu anaposhindwa rejesha fedha. 

Amesema kuwa kwa mwananchi au kikundi kukosa elimu ya mkopo wakati anachukua mkopo inaleta madhara wakati wa kurejesha hasa katika taasisi za mikopo zisizo rasmi, hivyo ni vema kila mwananchi akafika katika banda la self microfinance na kupata elimu na hata akikidhi vigezo pia kukopa.

"Kwahiyo tunachofundisha kwa kipindi hichi uulize maswali ya aina gani unapoenda kuomba mkopo na je uwe katika hali gani unaomba tu mkopo kabla ya kujua unataka kufanya nini au unajua unafanya nini ndo unaenda kuomba mkopo hicho ni kitu cha kuangalia", Amesema Meneja Masoko na uhamasishaji Linda. 

Amesema kuwa mwananchi anapofika katika banda la Self microfinance fund anapata elimu hiyo ya mikopo pamoja na vipeperushi vitakavyomsaidia hata baada ya maonyesho, ameongeza kuwa kupitia Wizara ya fedha kuna madarasa maalum yanayotolewa uwanjani hapo asubuhi na jioni kuhusiana na elimu ya fedha, akiba na uwekezaji. 

Aidha mpaka kufikia sasa self microfinance fund imetoa mikopo kiasi cha shilingi Bilioni 240 kwa wanufaika zaidi ya 200,000 , ambapo kiasi cha chini cha mkopo ni kuanzia shilingi 100, 000/= mpaka 500,000/= kwa kila mwana kikundi, kikundi cha watu watano wanaofahamiana na kwa mtu binafsi mwenye biashara anapewa mkopo kuanzia Milioni moja na kiwango cha juu ninBilioni. 

Self Microfinance fund ni mfuko ni mfuko ambao uko chininya Wizara ya Fedha kazi yake kubwa ni kutoa mikopo ys auna mbalimbali kwa wajasiriamali wadogo na wa kati , wafanyakazi wa serikali , Taasisi nyingine za fedha kama vile saccos, pia mikopo ya kuboresha makazi, wakulima, wavuvi na wafugaji.

Post a Comment

0 Comments