Muonekano wa Shule ya Moregas English Medium ya Kutwa na Bweni iliyopo kata ya Sirari Halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara.
Na Mwandishi Wetu Tarime.
Shule ya Msingi Moregas English Medium ya kutwa na bweni iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara imefanya vizuri matokeo ya mtihani wa darasa ka saba yaliyotangazwa hapo na Serikali.
Mwalimu mkuu shule Moregas English Medium, Paul Magabe amesema kuwa jumla ya wanafunzi 55 walifanya mtihani wa kumaliza mosomo ya darasa la saba kati ya 55 wanafunzi 44 wamepata wastani wa alama A masomo yote na Wanafunzi 11 wamepata wastani wa alama B.
“Nachukua nafasi hii kupongeza walimu na wazazi kuendelea kutoa ushirikiano ndiyo chanzo cha ufaulu”, amesema Mwalimu Paul.
Baadhi ya wanafunzi waliofanya vizuri katika shule wamesema kuwa jitihada kubwa zilizofanywa na walimu ndiyo zimesababisha kupata ufaulu mzuri katika masomo yote.
Mkurugenzi wa shule hiyo, Cosmas Mseti amesema kuwa suala la kutoa motisha kwa walimu wote pia ni chanzo cha kuongeza ufaulu kwa wanafunzi hao.
Cosmas ameongeza kuwa somo la TEHAMA nalo linachangia katika ufaulu na kueleza kuwa mwaka 2024 wanatarajia kuanza kufundisha masomo ya Kifaransa na Kichina hivyo sasa wazazi na walezi watumie fursa hiyo kuwapeleka watoto wao ili wapate elimu bora.
Aidha Mwalimu Daniel Wambura ambaye ni Mwalimu wa taaluma shuleni hapo amesema kuwa shule hiyo pia ina walimu wenye ubobezi mkubwa ndiyo chanzo cha ufaulu.
0 Comments