Ticker

6/recent/ticker-posts

RAIS DKT. MWINYI ATEMBELEA MRADI WA NYUMBA ZA FIDIA KWA WANANCHI WA BUMBWINI MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Viongozi mbambali wa Serikali alipowasili katika eneo la Bumbwini Kidazini Mkoa wa Kaskazini Unguja kutembelea Ujenzi wa Nyumba za Fidia kwa Wananchi wa Bumbwini, akiwa katika ziara yake kukagua ujenzi huo leo 24-11-2023 na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Hadidi Rashid Hadidi.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKUN inoyojenga nyumba hizo Bw.Ilhan Karadeniz, akitowa maelezo ya ujenzi wa Nyumba za Fidia kwa Wananchi wa Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja, alipofanya ziara kutembelea ujenzi huo leo 24-11-2023, na (kulia kwake) Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Mhe.Dkt.Khalid Salum Mohammed .(Picha na Ikulu)  
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo ya ujenzi wa Nyumba za Fidia kwa Wananchi wa Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya ORKUN Bw. Ilhan Karadeniz (kushoto kwa Rais) na (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Hadidi Rashid Hadidi, akiwa katika ziara yake kukagua ujenzi huo leo 24-11-2023.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiagana na Viongozi mbalimbali baada ya kumaliza ziara yake kutembelea Ujenzi wa Nyumba za Fidia kwa Wananchi wa Bumbwini Mkoa wa Kaskazini Unguja (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Hadidi Rashid Hadidi ,Mwakilishi wa Jimbo la Bumbwini Zanzibar Mhe. Mtumwa Peya Yussuf, Mbunge wa Jimbo la Bumbwini Zanzibar  Mhe. Mbarouk Juma Khatib na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Mohammed Said Dimwa.(Picha na Ikulu)

Post a Comment

0 Comments