Ticker

6/recent/ticker-posts

EQUITY BANK YAINGIA MAKUBALIANO NA SIMUSOLAR KUWAKOMBOA WAKULIMA NA WAVUVI KUPITIA PAMPU ZA MAJI ZA SOLA

BENKI ya Equity Tanzania Limited imesaini makubaliano na Kampuni ya uuzaji wa vifaa vinavyotumia nishati ya jua kwa wakulima na wavuvi nchini Simusolar Limited kwaajili ya kutoa pampu za maji za sola kwa wakulima wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 15,2023 Jijini Dar es Salaam kwenye hafla hiyo Mkuu wa Kitengo Cha Sheria Bw. Mboneko Mugisha amesema lengo la makubaliano hayo ni kusaidia wakulima wa Tanzania kufanya kilimo stahimilivu kinachotumia umeme wa jua katika umwagiliaji ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuongeza uzalishaji.

Amesema kuwa moja kati ya mikakati ya benki hiyo ni kuhakikisha wakulima nchini wanafanya kilimo biashara chenye tija hivyo basi benki imeingia makubaliano hayo ili kuhakikisha wakulima wanapata vitendea kazi vilivyobora vinavyotumia nishati ya jua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simusolar Bw. Michael Kuntz amesema kuwa makubaliano hayo yanalenga wakulima kuboresha na kurahisisha upatikanaji wa vitendea kazi kwenye maeneo ya uzalishaji na mwanga ambapo watajielekeza katika kuboresha kilimo chenye tija kupitia nishati jadidifu.

Post a Comment

0 Comments