Ticker

6/recent/ticker-posts

TGNP MTANDAO YATOA MAFUNZO YA MASUALA YA KIFEMINIA KWA MASHIRIKA NA KC KUTOKA MIKOA TISA NCHINI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) imeendesha Mafunzo ya Tathimini ya masuala ya Kifeminia kwa Mashirika yanayotetea haki za wanawake pamoja na wawakilishi wa Vituo vya Taarifa na Maarifa katika mikoa tisa nchini.
Miongoni mwa Mikoa hiyo ni pamoja na Kigoma, Shinyanga, Mara, Morogoro, Kilimanjaro, Mtwara, Dar es Salaam pamoja na mikoa mingine.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Desemba 19,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP, Bi.Lilian Liundi amesema kuwa mikoa hiyo wameichagua na kupata wawakilishi kushiriki mafunzo kutokana na mikoa hiyo kuwa na changamoto zinazohusiana na masuala ya ukatili wa kijinsia pamoja na masuala ya ushiriki hafifu wa wanawake katika uongozi.

“Tuliona mikoa hii inahitaji nguvu zaidi kwaajili ya kuhakikisha kwamba nayo inafikia hatua nzuri katika kupunguza au kutokomeza matukio ya ukatili pamoja na ushiriki mzuri wa wanawake katika uongozi”. Amesema Bi.Liundi.

Aidha amesema kuwa kwa mwaka mzima kazi kubwa imefanyika kwasababu tumeona hata kilele cha shughuli zote ambazo wamezifanya kwa mwaka mzima kwenye tamasha la Jinisia ambalo lilileta watu zaidi ya elfu mbili kutoka Wilaya zote Tanzania pamoja na nchi 17 kuwa na wawakilishi.

Amesema wanajipanga kwa mwaka ujao kuweka mikakati zaidi ili waweze kuoiga hatua zaidi wakifahamu yakwamba mwaka unaokuja una mambo mengi makubwa ambayo yanawahusu wao wadau wa masuala ya kijinsia.

“Mwaka unaokuja kuna uchaguzi wa Serikali za Mitaa, tunatamani kuona wanawake washiriki vizuri na waongezeke katika nafasi za uongozi kwenye serikali za mitaa”. Amesema

Kwa upande wake Mratibu wa Vituo Vya Taarifa na Maarifa upande wa Halmashauri ya Kasulu mkoani Kigoma, Bw.Josias James amesema kuwa kupitia mafunzo hayo wanategemea kutambua ufeminia kiundani zaidi ili kwenda kusaidia jamii ambayo imekuwa na changamoto katika kupata haki zao.

“Baada ya hapa tunategemea kwenda kubadilisha jamii, kuwa jamii ambazo hazitambui kila mtu anapaswa kupata haki ipi ili maisha yake yaweze kwenda vizuri”. Bw. James ameeleza

Nae Mwenyekiti wa Kituo Cha Taarifa na Maarifa Kata ya Kipunguni, Bi. Fatma Abdallhaman amesema kuwa ataendelea kuelimisha jamii katika kuondoa ukatili wa kijinsia, kutoa mafunzo ya biashara pamoja na mafunzo ya kilimo ili jamii iweze kuishi kwa usawa na kuondokana na masuala ya ukatili wa kijjnsia.

Post a Comment

0 Comments