Ticker

6/recent/ticker-posts

WANANCHI KIJIJI CHA MSOMERA WAOMBA KOUNGEZEWA HUDUMA YA MAJI.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akiongea na Brigedia Jenerali Hassan Mabena ambaye ni Kamanda Kikosi Kazi wa Mradi wa Ujenzi wa Nyumba 5000 kijiji cha Msomera.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akimshika mtoto wa jamii ya kifuhaji waliohamia hivi karibuni kutoka Ngorongoro kuja kijiji cha Msomera.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba (wa tatu kutoka kulia) akikabidhi moja ya mizinga ya kufugia nyuki, kwa jamii ya kifugaji katika kijiji cha Msomera.

***************

Na Hamida Kamchalla, HANDENI.


WANANCHI wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni, Mkoa wa Tanga wameiomba serikali kuwaongezea kiwango cha huduma ya maji ili kiendane na ongezeko la watu na mifugo kwa jamii ya watu wanaohamia kutoka katika Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro, mkoani Arusha.


Wameyamasema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba alipofanya ziara yake kijijini hapo ambapo hali hiyo imekuwa ikiwapa wakati mgumu linapokuja suala la kuwahamasisha wenzao waliopo Ngorongoro kuhamia katika kijiji hicho kwa hiyari.


"Maji yamekuwa ni ya shida, tunatumia maji ya kwenye bwawa ambayo siyo salama sana, na inatupa wakati mgumu sisi kama mabalozi tulioanza kuhamia hapa kuwahamasisha wenzetu kule kwasababu wanapokuja huku wanakumbana na shida ya maji, mtuanalie sana kwa ajili ya maji kwasababu tumeshakuwa wengi na ikibidi kuwekwe hata mradi wa maji" amesema Paulo Ngisaruni.


Aidha mbali na hilo wamesema kuna shida kwa upande wa elimu ambapo kutokana na wingi wa wanafunzi vyumba vya madarasa vimekuwa vichache lakini pia hakuna walimu wa kutosha hivyo wameingiwa na hofu ya uwezekano wa ufaulu kwa wanafunzi ambao kwa sasa wanakaa chini kutokana na ukosefu wa madawati.


"Sisi tuliotoka Ngorongoro, Mungu ametufungulia akili, watoto wetu wanakaa chini, ni aibu kwa shule hii iliyopewa jina la Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kukuta hakuna vyumba vya madarasa, mwalimu mmoja wa shule ya msingi utakuta anafundisha kuanzi darasa la kwanza hadi la saba,


"Tuna shaka na ufaulu hapa, tunakuomba mkuu wetu wa Mkoa, muangalie namna ya kupata madarasa, madawati lakini pia tupate walimu wa kutosha, wapo vijana wenye taaluma mbalimbali, ikiwezekana mfanye mpango hawa walimu walioko miongoni mwetu walipwe posho ili waendelee kufundisha wakisubiria ajira zao" ameendelea kusisitiza Ngisaruni.


Naye mkuu wa Wilaya ya Handeni Wakili Albert Msando amesema tatizo la uhaba wa maji linasababishwa hasa na ongezeko la watu na shuhuli za uzalisaji kwani awali walikuwa wakitegemea visima vinne lakini kutokana na matumizi mabomba yameunua.


Msando amebainisha kwamba hatua ya haraka ya muda mfupi wameiagiza Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA) wilayani humo kuhakikisha wanafanya linalowezekana wanapata mabomba ya haraka lakini pia wanaleta magari ya kubebea maji (maboza),


"Kwa hatua za muda mrefu, tumeshaanza mchakato wa kuleta maji kupitia mradi mkubwa ambao tutapata maji kutoka mto Ruvu, kwahiyo niiombe serikali kutuongezea nguvu ili tuupate kwa haraka mradi" amesema Msando.


Kufuata kero hizo, mkuu wa Mkoa wa Tanga Waziri Kindamba amesema kuwa serikali inafanya jitihada zake kuhakikisa kijiji ca Msomera kinaondokana na kero zote zilizopo kwakuwa inajua na ina mpango wa kuboresha zaidi mazingira na miundombinu na kukifanya kijiji hicho kuwa cha mfano.


Wakati mkutano huo ukiendelea jitihada za upatikanaji wa baadhi ya mahitaji hasa kwa upande wa elimu na ufugaji ziliendelea ambapo yalipatikana madawati 175, wakati kulikuwa na uhitaji wa madawati 160 na kufanya baking ya madawati 10.


"Natoa tathmini ya mkutano wetu, shida ya madawati tunaitatua hapahapa, tayari tuna madawati 175 yamepatikana, tulihitaji madawati 160, kwahiyo ziara ya madawati 10 mkuu wenu wa Wilaya atamikabidhi na mengine yatabaki ya akiba" amesema.


Lakini pia Wakala wa misitu nchini (TFS) ilikabidhi mizinga 33 ya nyuki kwa wafuaji na kutimiza mizina 133 kati ya 200 waliyoomba kupatiwa wafuaji hao ikiwa ni pamoja na fedha taslimu zilizotolewa na Jeshi la Wananchi nchini.


"Tunamikabidhi mizinga hii ya kisasa, mkafanye ufugaji wenye tija lakini nategemea mkatunze na kuyalinda mazingira na kwa yeyote mtakayemuona anaharibu mazingira mtoe taarifa kwa uongozi wa kijiji au ikibidi mum Kamati kwa mujibu wa sheria " amesisitiza Kindamba.

Post a Comment

0 Comments