Ticker

6/recent/ticker-posts

LINA PROFESSIONAL GOLF TOUR KULINDIMA MWISHONI MWA MWEZI FEBRUARI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

FAMILIA ya Nkya kwa Kushirikiana na Chama cha Wanawake wacheza Gofu Tanzania (TLGU) wamezindua mashindano ya Mchezo wa Gofu yanayoitwa Lina professional Golf Tour Proam ambayo yanatarajiwa kuanza rasmi mwisho wa mwezi Februari 2024,yenye lengo la kumuenzi Bi.Lina Nkya ambaye alikuwa mchezaji mahiri wa mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 15,2024 Makamu rais wa Tanzania Ladies Golf Union Bi. Hainy Magombe amesema kuwa Bi.Lina wakati wa uhai wake alikua ni mchezaji mahiri aliyeibeba bendera ya Tanzania kimataifa na kuongoza katika vitengo mbalimbali vya Uongozi wa Gofu kwa wanawake.

Kwa Upande wake Mhasibu wa TLGU Joyce Ndyetabura amesema wanatarajia mashindano hayo yatakuwa endelevu na kuimarika kwa miaka ijayo ambapo yanashirikisha vilabu mbalimbali ambavyo vimechaguliwa katika mikoa nchini.

Aidha amesema mashindano hayo yamegawanyika sehemu mbili ambapo yanahusisha wachezaji mahiri wabobezi wa mchezo huo na chipikizi wanaokua ambapo mwisho utawauhusisha wote kwa pamoja.

Pamoja na hayo amesema mashindano hayo yanafanyika katika vilabu tofauti tofauti kuanzia Februari 29,2024 Hadi Novemba 14-17,2024 ambapo itakua na wachezaji waliobobea zaidi ya 20 na wanaokua 75.

"Haya mashindano Tunaanza Februari 29-March 03,2024 katika Klabu ya TPC alafu mashindano yetu ya pili yataanza April 11-14, 2024 Sea Cliff Golf Club,alafu mashindano yetu ya tatu Julai 11-14 yatafanyika Arusha Gymkhana klabu,Alafu yatafata yatakayo anza Septemba 26-29 Arusha Moshi Klabu, alafu mashindano yetu ya mwisho yatafanyika Novemba 14-17, 2024 Dar es Salaam Gymkhana klabu". Amesema

Naye, mchezaji wa zamani wa Golf ambaye ni mume wa marehemu Lina Nkya, Bw. Said Nkya amesema kuwa zawadi zitatolewa kwa kiwango sawa kwa wachezaji waliobobea,heshimika na wale chipukizi ambapo bingwa atapata zaidi ya Dola Elfu moja za kimarekani.

Mashindano hayo yamelenga kuzalisha wacheza Gofu wabobezi ambao watakwenda kushindana katika mashindano makubwa ya Kimataifa,ambapo itakua fursa ya kuzalisha ajira kwa vijana.

Post a Comment

0 Comments