Ticker

6/recent/ticker-posts

MHANDISI MATINDI- HITILAFU KWENYE NDEGE AIRBUS A220-300 NI NDOGO NA LA KAWAIDA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la Ndege la Tanzania (ATCL) limesema tukio lililotokea katika ndege yake aina ya Airbus A220-300 iliyokuwa ikitoka Dar es Salaam kwenda jijini Mbeya kupata hitilafu kwenye moja ya injini zake kuwa ni dogo na la kawaida.

Mkurugenzi Mkuu wa ATCL, Mhandisi Ladslaus Matindi alipozungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi, Februari 29, 2024 jijini Dar es Salaam amesema ndege hiyo yenye namba 106 iliyoanza safari saa 12 jioni Jumamosi Februari 24, mwaka huu, ililazimika kukatisha safari na kurejea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam baada ya injini yake moja kupata hitilafu na kusababisha moshi ndani ya ndege.

"Kuna injini moja ilipata joto sana na ikawa na mafuta mengi ndiyo yaliyosababisha moshi ambao, uliingia kwenye mifumo ya hewa (AC) na ndiyo sababu moshi huo ukawafikia abiria sio ndege kuungua moto kama ilivyoelezwa," amesema

Hata hivyo,Mhandisi Matindi amesema hali ndani ya ndege hiyo haikuwa ya kutisha na marubani na wahudumu wengine walichukua hatua za kiusalama kwa kuwapa taarifa abiria na kuwasihi kuwa watulivu na wasiwe na wasiwasi.

"Hali ya moshi ndani ya ndege ilidumu kwa dakika tano tu na ilichukua dakika 25 ndege kurudi Dar es Salaam na abiria walibadilishiwa ndege na 104 kati ya 122 waliendelea na safari huku 18 wakiomba kubaAlipoulizwa kuhusu abiria kuvaa maski wakati wa tukio hilo, Matindi amejibu kuwa, "Hakukuwa na abiria aliyevaa maski wala kuzimia kama ilivyoelezwa."

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Mhandisi Matindi aliambatana na Mkuu wa usalama wa ndege za ATCL, Emmanuel Tivai ambaye amesema jambo lililotokea ni la kawaida kwa vyombo vya usafiri na kwamba, cha muhimu ni hatua zinazochukuliwa baada ya hapo.

"Inapotokea tatizo kama hilo hatua kadhaa huchukuliwa ikiwa ni pamoja na kurudisha ndege uwanjani ili iangaliwe na wahandisi wake na hicho ndicho kilichofanyika," amesema Tivai.

Kwa upande wa wahudumu wa ndani ya ndege hiyo, walisema walidhibiti taharuki ndani ya ndege kutokana na mafunzo bora waliyonayo huku rubani msimamizi wa ndege za Airbus ndani ya ATCL, akisema hatua muhimu zilifuatwa katika tukio hilo.

Post a Comment

0 Comments