Ticker

6/recent/ticker-posts

MKEMIA MKUU WA SERIKALI ATOA MSAADA WA VIFAA VYA MAABARA MAFIA

Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega (katikati) akikabidhi vifaa Kinga vya maabara kwa Kaimu Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka (kulia) baada ya kutoa mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali kwa shule ya Sekondari Kitomondo katika Wilaya ya Mafia Februari 1, 2024.
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo, Ayen Mathias, akiuliza swali kwa wawezeshaji katika mafunzo ya Usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani yaliyotolewa na Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali shuleni hapo.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo wakifuatilia mafunzo ya usimamizi na udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani kutoka kwa wawezeshaji kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (hawapo pichani).
Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Kanda ya Mashariki, Stanford Mwasilonda, akiwasilisha mada kuhusu madhara ya Kemikali kwa washiriki wa mafunzo ya matumizi salama ya kemikali.
Mtumishi wa Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki, Elice Omary (aliyesimama) akiwasilisha mada kuhusiana na alama mbalimbali za tahadhari za kemikali.
Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Sabanitho Mtega (kushoto) akiongea na walimu wa shule ya Sekondari Kitomondo baada ya kutembelea maabara ya Shule hiyo iliyopo wilayani Mafia.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kitomondo wilayani Mafia, Ramadhani Janabi (aliyesimama) akiwakaribisha timu ya wataalam kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali katika Mafunzo ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali za Viwandani na Majumbani kwa walimu na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo yaliyofanyika katika shule hiyo Februari 01 2024.

Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka (aliyekaa kulia), na Walimu wa Shule ya Sekondari Kitomondo baada ya kukamilisha mafunzo na utoaji msaada wa vifaa kinga vya maabara.
Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Bidhaa na Mazingira (aliyekaa katikati) akiwa pamoja na Kaimu Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Mafia, Mohammed Naboka (aliyekaa kulia), na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kitomondo baada ya kukamilisha mafunzo na utoaji msaada wa vifaa kinga vya maabara katika shule hiyo.

***************

Na Mwanaheri Jazza


Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali Imetoa mafunzo ya usimamizi na udhibiti salama wa kemikali pamoja na kugawa vifaa vya kujikinga wakati wa kufanya kazi za Maabara kwa wanafunzi na walimu wa sayansi katika shule ya Sekondari Kitomondo wilayani Mafia Mkoa wa Pwani.

Akizungumza wakati wa ugawaji wa vifaa hivyo, Mkemia kutoka Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Kanda ya Mashariki, Elice Omary, amesema utoaji wa vifaa hivyo utasaidia kuwakinga wanafunzi hao na athari mbalimbali zinazoweza kijitokeza wakati wakifanya mafunzo Kwa vitendo wawapo maabara.

"Tumepata fursa ya kuwapa elimu walimu na wanafunzi wa shule hii ya Kitomondo juu ya madhara yanayopatikana na matumizi mabaya ya kemikali na jinsi ambavyo wanaweza kujikinga, pia tumetoa baadhi ya vifaa Kinga Ili watakapokuwa wakifanya mafunzo kwa vitendo waweze kujikinga na athari mbalimbali zinazotokana na matumizi yasiyo sahihi ya kemikali" alisema Elice.

Kwa upande wake Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Kitomondo Ramadhan Janabi amesema vifaa Kinga hivyo vitasaidia walimu na wanafunzi kujikinga wakiwa katika mafunzo ya vitendo Kwa kuwa Maabara Kuna kemikali Hatarishi.

"Kwetu sisi huu msaada utasaidia sana Kwa kuwa tunafahamu maabara Kuna kemikali ambazo ni hatari kwa mwili wa binadamu, hivyo wanafunzi na walimu wanaofundisha watavaa na kuwa salama" alisema Mwalimu Mohamed.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo, Amina Athumani na Ayen Mathias wameishukuru Mamlaka kwa kuwapatia vifaa vya kujikinga wakati wakifanya mafunzo kwa vitendo".

"Tunaishukuru Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kwa kutuletea vifaa hivi kwani ni msaada mkubwa kwetu tutajikinga na kemikali hatarishi tukiwa maabara" walisema wanafunzi hao.

Post a Comment

0 Comments