Ticker

6/recent/ticker-posts

UKATILI WA KINGONO MASHULENI BADO UNAATHIRI WATOTO HASA WAKIKE

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

UKATILI wa kingono mashuleni bado unaathiri watoto hasa wakike pamoja na maneno makali kwa jinsia zote ambapo imesababisha wanafunzi kuona shule kuwa sio eneo salama,

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam Machi 14,2024 Mratibu wa My Legacy Amina Ally wakati wa kikao kazi kinachofadhiliwa na mfuko wa Uwezeshaji wanawake (WFT) ambacho kimeshirikisha wadau wanaopinga vitendo hivyo kutoka taasisi ya mbalimbali nchini.

Amesema wamekutana kutengeneza mazingira salama ya kujifunzia watoto wanapokuwa shuleni kwa lengo la kuunda waraka kwaajili ya watunga sera kutambua jambo hilo ili kuhakikisha inaundwa sheria kuondoa changamoto hiyo.

"Takwimu bado zinaendelea kusema ukatili wa kijinsia bado unaathiri mashuleni hasa watoto wa kike wamejikuta wakiwa wahanga wa ukatili wa kingono na wakiume wamejikuta wakifanyiwa ukatili wa kimwili". Amesema.

Kwa upande wake, Mratibu mradi wa Taasisi ya TAI TANZANIA, Mariam Mitanga amesema wanatumia Teknolojia ya Katuni chapa tatu (3D Animation film) kutoa elimu kwa wanafunzi kuhusiana na madhara yanayopatikana kutokana na ukatili na sehemu ya kwenda kuripoti inapotokea wamefanyiwa vitendo hivyo.

Naye, Katibu wa SMAUJATA wilaya ya Kinondoni, Fatma Issa amesema wameshiriki katika kikao kazi hicho kupata wazo la pamoja namna ya kupiga vita vitendo vya ukatili mashuleni, ili kumjengea mwanafunzi mazingira salama ya kujifunzia.

Post a Comment

0 Comments