Ticker

6/recent/ticker-posts

WAZIRI JAFO APOKEA GARI KWA AJILI YA OFISI KUTOKA WFP

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo amesema Serikali ya Tanzania inathamini mchango wa wadau katika kuleta maendeleo ya nchi.

Ametoa kauli hiyo wakati akipokea gari kwa ajili ya shughuli za Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo Machi 19, 2024 katika Mji wa Serikali, Mtumba jijini Dodoma,

Akimshukuru Mwakilishi Mkazi wa WFP Bi. Sarah Gordon-Gibson, Dkt. Jafo amesema Serikali inafarijika kufanya kazi na wadau mbalimbali wa maendeleo ambao wamekuwa msaada mkubwa kwa shughuli za Serikali.

Amesema kuwa gari lililotolewa na shirika hilo litasaidia katika shughuli za Ofisi hususan katika kuwahudumia wataalamu katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku yakiwemo kutembelea na kukagua miradi ya mazingira inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali nchini.

Pamoja na hayo, Waziri Dkt. Jafo ametoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuzisaidia taasisi zingine za Serikali kwa kuzipatia vitendea ili ziweze kutekeleza majukumu yao.

“Nipende kuwashukuru WFP kwa kufanya kazi pamoja na sisi (Ofisi ya Makamu wa Rais) na Serikali kwa ujumla na niwaombe tuendeleze ushirikiano wetu kwa mustakabali wa taifa,“ amesisitiza.

Kwa upande wake Bi. Sarah amesema kuwa makabidhiano hayo ya gari ni kusherehekea ushirikiano baina ya shirika hilo na Serikali ya Tanzania kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais.

Amesema kuwa anafarijika pia kushiriki katika hafla hiyo ya makabidhiano ya gari hilo na kuongeza kuwa litaisaidia watendaji wa Ofisi kuweza kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Bi. Sarah amemshukuru Waziri Jafo na watendaji wa Ofisi yake kwa kudumisha ushirikiano na Shirika la WFP katika shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwemo za hifadhi ya mazingira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikata utepe kuashiria kupokea gari lililotolewa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Pembeni ni Mwakilishi Mkazi wa WFP Bi. Sarah Gordon-Gibson na wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais) Bi. Christina Mndeme.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikata utepe kuashiria kupokea gari lililotolewa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Pembeni ni Mwakilishi Mkazi wa WFP Bi. Sarah Gordon-Gibson na wa pili kushoto anayeshuhudia ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais) Bi. Christina Mndeme.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akikagua na kuendesha gari lililotolewa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) leo Machi 19, 2024. Anayemhudia ni Mwakilishi Mkazi wa WFP Bi. Sarah Gordon-Gibson.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akitoa shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) mara baada ya kupokea gari jijini Dodoma leo Machi 19, 2024.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) Bi. Sarah Gordon-Gibson mara baada ya kukabidhiwa gari kwa ajili ya matumizi ya Ofisi ya Makamu wa Rais kutoka shirika hilo leo Machi 19, 2024 jijini Dodoma. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu (Mazingira) Ofisi ya Makamu wa Rais) Bi. Christina Mndeme na kulia ni Naibu Katibu Mkuu (Muungano) Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Abdallah Hassan Mitawi.

Post a Comment

0 Comments