Ticker

6/recent/ticker-posts

JUKWAA LA UUNGANISHAJI MASOKO LAWAKUTANISHA ZAIDI YA WASHIRIKI 200 MANYARA

Zaidi ya washiriki 200 kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Manyara wamekutana katika Jukwaa la Uunganishaji wa Masoko lililoandaliwa na Hand in Hand Eastern Africa Tanzania kwa lengo la kuwaunganisha wazalishaji na wanunuzi ili kuwapatia fursa za masoko.

Akizungumza katika jukwaa hilo lililofanyika Juni 19, 2026 katika Hoteli ya White Rose mkoani Manyara, Meneja wa Tawi la Hand in Hand Mkoa wa Manyara, Bw. Yona Ona, amesema upatikanaji wa masoko ni daraja muhimu kati ya uzalishaji na ongezeko la kipato kwa wananchi.

“Jukwaa hili ni daraja kati ya uzalishaji na kuongeza kipato kwa kuwa linawakutanisha wazalishaji na wanunuzi moja kwa moja,” amesema Bw. Ona.

Jukwaa hilo ni sehemu ya jitihada za Hand in Hand Eastern Africa Tanzania za kuwafungulia wanufaika wake fursa za masoko na kuwawezesha kuongeza kipato kupitia shughuli za kiuchumi.

Post a Comment

0 Comments