Ticker

6/recent/ticker-posts

AMEND,USWIS KUTOA MAFUNZO ELIMU USALAMA BARABARANI AWAMU YA PILI JIJINI DODOMA

Na Mwandishi Wetu

SHIRIKA la Amend linaendelea na mkakati wake wa kutoa elimu kwa waendesha vyombo vya moto hususani pikipiki kukabiliana na tatizo la ajali za barabarani.

Shirika hilo kwa kushirikiana na Ubalozi wa Uswisi nchini Tanzania wamepanga kuendeleza mafunzo ya elimu ya usalama kwa waendesha pikipiki (Bodaboda) jijini Dodoma hususani kwa maeneo ambayo hayakufikiwa awali.

Akizungumza kuhusu mafunzo hayo, Msaidizi wa Miradi kutoka Shirika la Amend, Amiri Matimba amesema kuwa yataanza kutolewa Aprili 15, mwaka huu katika kata ambazo hazikupata mafunzo hayo yapotollewa Februari mwaka huu.

Amesema kuwa mafunzo hayo yananalenga kuboresha usalama wa waendesha pikipiki, abiria na watumiaji wengine wa barabara, hivyo kuzuia vifo na majeruhi wa matukio ya ajali ambapo wengi wao ni vijana.

"Ombi la mkuu wa wilaya limekubaliwa na mafunzo hayo yataanza rasmi April 15 yakitolewa na shirika la Amend kwa ufadhili wa ubalozi wa Uswis, hapa Dodoma na yanalenga kata ambazo hazikupata mafunzo hayo hapo awali," amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Walimu wa Usalama Barabarani, Mwalimu Massava Ponera amewataka maofisa usafirishaji kujitokeza kwa wingi kupata elimu hiyo ambayo ni muhimu kwa shughuli zao.

Ameeleza mafunzo ya elimu ya usalama barabarani yana umuhimu makubwa kwani mbali na vifo ajali za barabarani husababisha ulemavu wa kudumu huku takwimu za sensa nchini zikionesha kuwa asilimia kubwa ya Watanzania ni vijana na wengi wameamua kujikita katika ujasiriamali wa bodaboda.

Februari 2024 yalihitimishwa mafunzo ya awali kwa maafisa usafirishaji 250 katika hafla ya ufungaji mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Alhaji Jabir Shekimweri.

Mkuu huyo wa wila katika hotuba yake aliuomba ubalozi wa Uswis nchini kama utaridhia udhamini mafunzo mengine kwa kata ambazo Amend hawakuzifikia kuendeleza ufikishaji wa elimu hiyo.


Post a Comment

0 Comments