Ticker

6/recent/ticker-posts

EQUITY BANK YAZINDUA DIRISHA LA WANAWAKE- MWANAMKE PLUS

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BENKI ya Equity imezindua Dirisha la Wanawake - Mwanamke Plus ambalo ni mpango maalum unaolenga kuwainua wanawake katika sekta ya biashara na uchumi ambapo natoa fursa za kipekee za mikopo, bima, mafunzo ya biashara, na huduma za ushauri, ikiwemo uwezeshaji wa kidigitali kupitia Equity Mobile na huduma za kibenki mtandaoni.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na wanawake zaidi ya 200 leo Mei 20, 2024 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima amesema dirisha hilo litasaidia kuleta uchechemuzi katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu na biashara pamoja na kuongeza kuongeza uelewa kwa wanawake kuhusu ujumuishi wa kifedha na jinsi ya kukuza mitaji yao huku akitoa rai kwa benki hiyo kuleta huduma zinazomjumuisha mwanaume.

Amesema takwimu zimeonesha kuwa Tanzania ni miongoni mwa Nchi yenye idadi ndogo ya wanawake wanaotumia teknolojia katika sekta ya fedha huku serikali ikichukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hiyo ikiwemo kuhamasisha matumizi ya pesa kidigitali.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji benki ya Equity Bi Isabela Maganga amesema mahitaji ya mikopo kwa wanawake nchini ni zaidi ya trilioni 4.4 ambapo kwa sasa hayajafikiwa na taasisi za kifedha hivyo dirisha la mwanamke plus itasaidia kuyafikia makundi hayo.

Nae mchumi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika –AFDB, Bw. Prosper Charle amesema benki hiyo imeendelea kuweka kipaumbele kwa wanawake ili kuleta uhimilivu toshelezi wa uchumi pamoja na kung’amua fursa zilizopo katika jamii.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dirisha la Wanawake - Mwanamke Plus ambalo ni mpango maalum unaolenga kuwainua wanawake katika sekta ya biashara na uchumi uliofanyika katika hoteli ya Serena leo Mei 20, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji benki ya Equity Bi Isabela Maganga akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dirisha la Wanawake - Mwanamke Plus ambalo ni mpango maalum unaolenga kuwainua wanawake katika sekta ya biashara na uchumi uliofanyika katika hoteli ya Serena leo Mei 20, 2024 Jijini Dar es Salaam
Afisa Mwendeshaji- Jubilee Life Corporation of Tanzania Limited, Esther Swai akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dirisha la Wanawake - Mwanamke Plus ambalo ni mpango maalum unaolenga kuwainua wanawake katika sekta ya biashara na uchumi uliofanyika katika hoteli ya Serena leo Mei 20, 2024 Jijini Dar es Salaam
Mchumi kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika –AFDB, Bw. Prosper Charle akizungumza wakati wa uzinduzi wa Dirisha la Wanawake - Mwanamke Plus ambalo ni mpango maalum unaolenga kuwainua wanawake katika sekta ya biashara na uchumi uliofanyika katika hoteli ya Serena leo Mei 20, 2024 Jijini Dar es Salaam
Matukio ya picha mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Dirisha la Wanawake - Mwanamke Plus ambalo ni mpango maalum unaolenga kuwainua wanawake katika sekta ya biashara na uchumi uliofanyika katika hoteli ya Serena leo Mei 20, 2024 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Post a Comment

0 Comments